WATAKIWA KUTUMIA KINYESI CHA BINADAMU KUTENGENEZA GESI




Mkuu wa mkoa wa Manyara bwana Elastone Mbwilo ametoa ushauri kwa
wakulima,wafugaji pamoja na wavuvi kote nchini amewataka kuanza
kutumia kinyesi cha binadamu katika kutengeneza bioges.

Mbwilo aliyasema hayo wakati alipokuwa akitembelea katika sehemu
mbalimbali za wakulima nanenane katika viwanja ya themi vilivyoko eneo
la njiro jijini Arusha,ambapo ilieleza kwamba ni wakati sasa wa
wananchi kuwa na mabadiliko katika kuzalisha mbinu mpya ambapo kauli
mbiu ilikuwa ni''zalisha mazao ya kilimo na mifugo kwa kulenga
mahitaji ya soko''

Alieleza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakitumia kinyesi cha wanyama
bila kufanya mabadiliko ,na kwamba hiyo yote ni kwa sababu ya kutojua
kuwa kinyesi cha binadamu kinaweza kutengeneza bioges na kuzalisha
umeme.

Bwilo alifafanua kuwa kinyesi cha binadamu ni kinyesi ambacho
kinazalisha bioges kwa wingi na kwamba ni rais kupatikana muda wote
kulingana na familia kuwa nyingi katika jamii tofauti na wanyama kwani
imwkuwa tofauti kwa kipindi hiki wanyama wengi wamekuwa hawashibi
hivyo kushindwa kutoa kinyesi kingi,hivyo na kueleza kuwa wananchi
kutumia vyoo vyao kuzalisha bioges.

Mbali na hayo Mbwilo aliendelea kuwapongeza wakulima wote
waliojitokeza katika maonyesho hayo kwani walijitokeza kwa wingi
kulima na kufuga ikiwa ni pamoja na uvuvi wa samaki kwani waliweza
kuonyesha mazao mbalimbali tofauti na zamani ambapo walikuwa
wakionyesha aina moja ya mazao.

Pia alibainisha kuwa anawapongeza wakulima hao kwa kuenda na nyakati
za majira kulingana na kubadilika kwani aliona wengi wao walikuwa na
wabunifu na waelewa kwani nyakati hizi zimekuwa zikibadilika kutokana
na nyakati,na kwamba zamani mvua zilinyesha kwa wakati huku wakulima
wakiwa na ratiba pamoja na matumaini ya mazao yao kupendeza tofauti na
sasa mvua zimekuwa hazinyeshi kulingana na muda,na kusema kwamba laki
ni kupitia changamoto hiyo wakuima wameweza kuweka kipaumbele
umwagiliaji na kwamba kupitia hali hiyo balaa la njaa halitakuwepo.

Hata hivyo Mbwilo ailieleza kuwa wakulima hawna budi ya kuwa
wavumilivu huku wakihakikisha wanajiunga kwenye mashamba darasa ili
waweze kuwa na uelewa mkubwa katika kilimo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wanawaandaa wakulima wao kutoka kila wilaya ambao wako
vijiji vyao ili waweze kuja kutembelea na kuangalia maonyesho hayo.

Alisema kuwa kulingana na takwimu jinsi zinvyoonyesha wakulima kwa
mwaka huu katika ufunguzi hawajajitokeza jambo ambalo limeshindwa
kueeweka tatizo lilikuwa ni nini hivyo na kuwataka wawalete wenzao na
kuanza kujadili ni jinsi gani kukuza masoko.

Nae mkuu wa wilaya ya monduli Josia Kasunga aliweza kuweka bayana kwa
kueleza kwamba wakulima hao kwa mwaka huu hawakujipanga sawasawa
tofauti na miaka ya nyuma na kuwa wengi wao wamechelewa kutengeneza
vibanda wengine wakiwa na visingizio visivyokuwa na sababu.

pia kwamba kuptia hali hiyo halimashauri zote na viongozi kwa ujumla
hawana budi kuwa msitari wa mbele katika kuhamasisha wananchi wote
bila kuwa na visingizio visivyokuwa vya msingi kwani  wakulima
kutohudhuria kwa ni moja ya sababu ya viongozi hao kutowahamasisha
wananchi,hivyo hali hiyo kuwa mwanzo na mwisho kwani wanajenga taswira
mbaya kwa wananchi kwani kuna hata baadhi ya halimashauri zimechelewa
kwenye maonyesho hivyo wakati mwingine kutorudia hali hiyo.

Hata hivyo kwa alisema kuwa kwa mwaka kesho hali hiyo haitajitokeza
kwani kila halmashauri na viongozi wote wa taso watakaa na
kumpendekeza mtu mmoja ambaye atafanya shughuli nzima ya kuhamasisha
wananchi huku wakipita mitaani na magari ya matangazo juu ya sherehe
za wakulima nanenane kwani imebainika kuwa wananchi wengi hawakujua
suala hilo na uenda ndio moja ya  sababu ya kutokuwepo kwa wannchi
hao,hivyo kiongozi huyo atakuwa na kibali maalumu cha kufanya kazi
hiyo .

pia alizidi kuongelea mapungufu yaliyokuwepo na kuwatupia lawama
baadhi ya wakulima kwa kusema kuwa hawakujiandaa mapema katika kilimo
chao kwani kuna wengi wao mazao bado hayajakomaa kama mimea kwani kuna
mimea mingine ndio inaota,na kwamba hayo sio maonyesho kwani mgeni
akifika kwenye bustani yake akiwa na lengo la kujifunza mmea huo baada
ya kustawi hivyo itakuwa ngumu kumueleza mpaka kukuelewa,na kwamba
kama ni hivyo basi wajitahidi kuweka  gred ya vitaru tofauti ambapo
itaonesha kila hatua ya ukuaji wa mimea hiyo ili kumjenga mwananchi
kiuelewa zaidi na kuyatambua mazao hayo.

alisema kuna baadhi ya wkulima,wafugaji pamoja na wavuvi wamekuja
kwenye maonyesho kwa ajili ya biashara na kuemea bidhaa,jambo ambalo
limekuwa kinyume kabisa na utaratibu unavyokuwa ukilinganisha na miaka
mingine ya nyuma.

Nae mkuu wa wilaya Moshi Ibrahim Msengi aliweza kubainisha kuwa baadhi
ya wakulma hawakujitokeza kwa wingi kufuatia ukosefu wa elimu kwa
wananchi hao juu ya sherehe hizo za nanenane.

alisema ni vizuri taso iweke vipeperushi kila sehemu inayozunguka
jamii ikiwa ni pamoja ya kuwepo sura ya taasisi kwa wale waliofika
kwenye maonyesho kuoewa semina hizo juu ya kilimo.

Lakini tu alisema pia magonjwa mengi yaliyoikabili jamii imechangia
wakulia kutojitokeza katika sikukuu hiyo,hivyo kupelekea
kutojishughulisha  na kilimo na hatimaye kuchelewa maonyesho.

Ibrahim alisema katika wilaya yake ya kilimanjoro kuna wataalamu wa
afya ambapo wamekuja kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango,kwa
wananchi,jinsi ya kupangilia muda na hatimaye kufanikisha,

Akielezea umuhimu wa semina hizo Elvasta Mshana ambaye ni mratibu wa
afya ya uzazi na mroro wilaya ya moshi alisema lengo ni kuwaelimisha
wakulima kuwa pale watakapo kuwa na afya pamoja na kutumia njia za
uzazi wa mpango wataweza kupangilia kilimo chao kwa hali ya ustadi
kabisa.


Nae mwenyekiti wa Taso mkoani Arusha bw.Uther Kitonga alibainisha
kwamba  taso ilianza mnamo mwaka 1993hapa kanda ta kaskazini katika
viwanja vya TRA ambapo kwa mwaka huu ilitimiza miaka 20 ambapo tiyari
mafanikio ni mengi kama kuboresha miundo mbinu kama barabrara,vibanda
vya kudumu pamoja na maji na umeme hivyo kupelekea kazi sikukuu ya
wakulima kwenda vizurri kabisa.

kitonga alisema kwamba mbali na mafaniko wao kama Taso wanazo
changamoto kubwa kwamba seikali haitengi ela za kutosha katika
kuendesha shughuli mpya z sikukuu hizo za nanenane,huku wakipewa ela
ndogo na kusababisha kutofanikiwa malengo yao kwa kina.

Alibainisha kwamba halmashauri katka wilaya zote zinatakiwa kuwa mfano
bora na kiini kikuu katika kufanya ushindani wa kilimo.

Alieleza kuwa Taso na serikali kwa ujumla wanayo ndoto ya kuanzisha
chuo cha kiimo ndani ya viwanja vya Taso ambapo itahusisha wanafunzi
mbalimbali wanaojihusisha na kilimo,uvuvi,biashara pamoja na mifugo
,lengo likiwa kutaka eneo la viwanja kutokaa bila kutumika wakisubiria
sikukuu za nanenane,hivyo hali hiyo itasaidia wakulima kuendeleza
kilimo chao mwaka hadi mwaka mpaka kufikia sikukuu hizo,ambapo
wanafunzi hao watjifunza kwa vitendo zaidi.

Kwa upande wa Afisa kilimo kutoka wilaya ya babati vijijini Edga
Lyakurwa alieleza kuwa wao walikuja na technolojia mpya ya kuwapa
elimu wakulima kutumia njia mbalimbali za kilimo na umwagiliaji wa
dawa za kuulia wadudu katika mashamba yao kwenye maonyesho hayo ya
sikukuu za nanenane.

Alizitaja technolojia hizo kuwa ni kutumia fagio la kisasa la kuuwa
wadudu ambalo hutumika kupiga dawa na kuuwa wadudu walioko kwenye
magugu tofauti na zamani ambapo wananchi wengi na wakulima walitumia
mabomba huku wakiwa wamevaa mgongoni na kutumia nguvu lakini kupitia
technolojia hiyo mpya ya kutumia fagio na rahisi na ni bora kwa
watumiaji.

Afisa huyo alisema kwamba wakulima wake kupitia kilimo wamekuwa na
mafanikio makubwa sana kwani wameweza kujenga majumba mazuri,kusomesha
watoto shuleni,kujenga afya zao ikiwa ni pamoja na kutotegemea
serikali katika kuwapatia msaada wa chakula.

Edga alibainisha kuwa anaiomba serikali kuwaboeshea miundo mbinu haswa
kwenye sekta ya viwanda vya usindikaji ili wakulima waweze kuongeza
dhamani yao na kwamba wananchi  wawe tiyari kupokea tachnolojia mpya
ikiwa ni pamoja na kusikliza ushauri wa wataalamu.


 Hata hivyo Edga alisema bado wanazochangamoto kwa wakulima wake kuwa
ni pamoja na wao kutopenda kujiunga kwenye kwenye vikundi vya darasa
kupata elimu,kuosekana kwa mbinu rafiki kama uzalishaji,kwani hukosa
pa kupeleka mazao yao kwenye masoko na viwanda vya usindikaji,upungufu
wa wataalamu hivyo kutotosheleza,usafiri wa kwenda kuwafikia wakulima
na maeneo husika,ikiwa ni pamoja na mabadiliko nchi.

Na kwa upande wa wakulima,wafugaji pamoja na wavuvi walihudhulia
kwenye sikukuu ya maonyesho ya wakulima katika viwanja hivyo vya
nanenane themi njiro waliweza kueleza changamoto mbalimbali
wanazokumbana nazo nz jinsi gani serikali ingeweza kuwasaidia.

Walisema kwamba wanakabiliwa na ukosefu wa mitaji ya kutosha katika
kuendesha kilimo,ikiwa ni pamoja na kukoswa masoko ya kwenda kuuza
mazao yao hivyo na kuiomba serikali waweze kuwawezsha katika sekta
hizo ili waweze kuinua kilimo chao na mwisho kuwa kimataifa.

Mmoja wa wakulima kwa jina la Didas Emil Mallya yeye ni mkulima kutoka
wiliya ya moshi ambaye anajihusisha na kilimo cha kahawa alisema kuwa
kuna changamoto kuwa ni udogo wa ardhi kutotoshereza hivyo kupelekea
mikahawa kutoenea kwenye ardhi.

Pia alifafanua kuwa changamoto nyingine ni bei kuwa ndogo pamoja
ukosefu wa mashine za kumenyea kahawa ili kupata kahawa bora ili
kuweza kupata kahawa nzuri,hivyo na kuiomba serikali kuwaangalia ili
waweze kuboresha kilimo chao cha kahawa pomoja kilimo kingne.

Na kwa upande wa mmoja wa mwananchi aliyefika kwenye viwanja hivyo
alisema kwamba taso imeweka gharama kubwa ya kiingilio hivyo kupelekea
baadhi yao kushindwa kuingia,ambapo alibainisha kwamba ni ngumu mtu
kuaharribu nauli zaidi ya elf mbili na ambapo huko nanenane hakuna
kazi anayoenda kuzalisha hivyo kuamua kuacha wakidai hakuna faida

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post