KWA WALE WANAOTAKA KUMUONA LADY JAY DEE (ANACONDA) NA PROFESA J RATIBA HII HAPA

 

Kwanza tunapenda kuwafahamisha wakazi wa Arusha kuwa tuko mjini kwenu tayari.

Pili ni kuwapa ratiba nzima ya jinsi gani tunaweza kuonana na kubadilishana mawazo, huku kila alie shabiki wa muziki apate kitu anachokipenda kwa roho safi.

Leo siku ya Jumatano 7 August 2013.
Kutakuwa na zoezi la ku sign autographs kwa watakaonunua CD Album ya Lady JayDee "Nothing But The Truth"
Zoezi hilo litafanyika Mount Meru Hotel, kuanzia saa 11:00jioni hadi saa 2:00 usiku
Time hizo kwa kizungu ni 5:00PM to 8:00PM

Siku ya alhamisi tar 8 August 2013, zoezi hilo litaendelea huku likiambatana na Tshirts za Team Anaconda
Kuanzia saa 4:00asubuhi mpaka saa 7:00mchana
(Yaani 10:00AM -1:00PM)

CD Album inauzwa kiasi cha sh: 5,000/= za kitanzania
Na Tshirt moja inauzwa kiasi cha sh:15,000/= za kitanzania


Shows zitakuwa kama ifuatavyo:

EID MOSI: Tripple A kuanzia saa 3:00 usiku ambapo Lady JayDee, Prof Jay na Machozi Band watakuwepo kukupatia JOTO HASIRA kupunguza baridi la Arusha.

EID PILI: Bortanic Garden kuanzia saa 6:00 mchana hadi 12:00 jioni Lady JayDee na Machozi Band watakuwepo kuburudisha familia na watoto na kuifanya siku iwe nzuri kabisa.




EID PILI USIKU: Snow View Hotel - Bomang'ombe kuanzia saa 3:00usiku Prof Jay na Lady JayDee watamaliza na wewe sikukuu kwa show kali
 
Karibuni tujumuike kwa pamoja

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post