Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama
Rose Haji Mwalimu akitoa mada kwa wadau wakati wa warsha ya Mameneja
na Wakurugenzi wa redio za jamii kuhusiana na umuhimu wa kutengeneza
vipindi vyenye ubora vitakavyovutia jamii wakati wa warsha
ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na
Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza ambayo imefadhiliwa na
UNDP na kuratibiwa na
UNESCO.
Mwezeshaji kutoka Search for Common Grounds
Patricia Loreskar akizungumza na Mameneja wa redio za jamii nchini
kuhusiana na shirikika lake linavyofanya kazi ya kutoa Elimu kujenga
Amani na kutatua migogoro mbalimbali inayojitokeza kwenye jamii yetu
na kuwataka redio za jamii zisiwe chanzo cha kuvuruga Amani bali zitoe
Elimu ya kudumisha Amani kwa jamii nchini kwenye warsha ya
wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha
Sengerema FM kwa redio za jamii nchini kwa ajili ya
kujiandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi
wa mwaka 2015.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano
na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin akifafanua
jambo wakati wa warsha ya wiki moja ya Majadiliano baina ya Vyombo vya
habari vya kijamii (redio) na nafasi yake katika kuhamasisha
Demokrasia na Amani kwenye mazingira shirikishi na umuhimu wake katika
kuunganisha jamii na kutatua migogoro ikiwa ni moja ya jitihada za
kuendeleza Elimu haswa katika kuboresha sera za uhariri wa
habari.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Mameneja na
Wakurugenzi wa redio za jamii wakifuatilia mada mbambali zilizokuwa
zikitolewa kwenye Warsha ya wiki moja inayoendelea katika kituo cha
Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani
Mwanza.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Grace Mapunda akizungumzia uhusiano
wao na redio ya jamii Sengerema FM ambao amesema redio hiyo imekuwa
mchango mkubwa sana kwa wananchi wa wilaya hiyo katika kupashana
habari.
Meneja wa Redio Jamii ya Orkonerei Fm ya
Wilayani Simanjiro Khadija Abdallah akiwasilisha mada kwenye warsha ya
wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoa wa
Mwanza.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye
pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy akielezea
umuhimu wa kufanya utafiti kwa redio za jamii kwa ajili ya kuboresha
usikivu na vipindi vyao kwa jamii.
Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO
Adeline Lweramula akichangia maoni yake wakati wa kujadili
uboreshaji wa sera za uhariri wa habari. Kulia ni
mwezeshaji Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano
na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph
Al-Amin.
Meneja wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney
Ivins (kushoto) akibadilishana mawazo na wadau wa Search for Common
Grounds wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha
Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani
Mwanza.