HAYA SASA MASHABIKI WA KANDANDA NCHINI SASA KUBOFYA *149*31# KUPATA MATOKEO NA RATIBA ZA LIGI MBALIMBALI ULIMWENGUNI.

20130817_132318
Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni Afrisoft Technologies Ltd Brian Mushi, Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni hiyo David Kagoma pamoja na Msimamizi wa Fedha Bw. Bujune Leo kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-soka.
Na. Mwandishi wetu.
Kampuni ya Afrisoft Technologies Ltd inayojihusisha na masuala ya teknolojia zinazorahisisha maisha ya kila siku, sasa imekuja na huduma mpya ya ‘M-Soka’ ambapo mtumiaji wa mtandao wa Vodacom anaweza kufaidi huduma hiyo kwa muda wowote na kwa haraka zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Brian Godwin Mushi amesema wameamua kutengeneza huduma hiyo, kwa kuwa mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana na watu wengi na hivyo ukizingatia mahitaji ya watu kutaka kujua matokeo au kujua ratiba, sasa haina haja tena kusubiri gazeti au redio ila ukiingia katika ‘M-Soka’ (Mobile Soka)unapata kila kitu moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi.
Bw. Mushi amesema ukizingatia hali halisi sio kila mahali panapatikana huduma ya intaneti na sio kila mtu ana simu inayoweza kuunganishwa kwenye mtandao huo, hivyo kupitia ‘M-Soka’ unaweza kupata matokeo au ratiba kwa kutumia simu ya aina yeyote ile.
Akitaja namba zinazotumika kupata matokeo hayo amesema kuwa ni *149*31# kwa gharama nafuu ya shilingi 40 tu.
Amesema unaweza kupata matokeo ya mechi zilizochezwa, ratiba ya mechi zitakazofuata na pia msimamo wa ligi mbalimbali, na kuwa kama ni matokeo unaweza kupata ya leo, jana, juzi na siku moja kabla na kama ni ratiba utapata ya leo, kesho, keshokutwa na mtondogoo na kama ni msimamo unapata wa wakati huohuo(real Time).
Pia kuna ‘option ya live’ ambayo inakuwezesha kufuatilia mpira kwa dakika hiyo hiyo hata goli likifungwa inakupa matokeo yake mpaka jina la mfungaji na dakika ambayo goli limefungwa.
Ni njia rahisi kwa mashabiki kufuatilia matokeo ya timu yao wanayoipenda na kupata taarifa ya kila kitu ikiwemo magoli, kadi hata penati.
Ligi zinazopatikana katika mtandao huo ni za Uingereza, Hispania, Ufaransa, Italia, Ujerumani, UEFA, Kombe la Dunia na CAF kwa shilingi 40 tu.
Kwa mshabiki yeyote wa soka usipate tabu, chukua simu yako na uandike *149*31# na upate matokeo, ratiba na msimamo papo hapo bila shaka na kwa gharama nafuu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post