Ticker

6/recent/ticker-posts

NAPE KUTENGUA MAAMUZI YA HALIMASHAURI KUU YA CCM KAGERA YA KUWAFUKUZA MADIWANI NA KUWAFUTIA NYADHIFA ZA UDIWANI

       Diwani Alexander Ngalina wa Kata Buhembe na Naibu Meya
            Diwani Richard Gaspar wa Kata ya Miembeni na mjumbe mkutano mkuu wa Taifa wa CCM
             Diwani  Dauda Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo
              Diwani Samweli Ruangisa  wa kata ya Kitendaguro
                 Diwani  Deusdedith  Mutakyawa kata Nyanga
   Diwani  Yusuf Ngaiza wa kata ya Kashai na mwenyekiti wa CCM Bukoba mjini
               Diwani Robert Katunzi wa kata ya Hamugembe
    Diwani Murungi Kichwabuta wa viti maalum na mjumbe baraza kuu la Taifa la wanawake
                      Hongereni sana jamani....
  Ni furaha kwa wanachi wa manispaa ya Bukoba baada ya Nape kutangaza
                    Murungi akitabasamu
                         Ni furaha kila pembe
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa Abdul Kagasheki akiwa na wananchi mbalimbali  wakifurahia kauli ya Nape
     Wanachi wakishangilia kauli ya Nape
                                                
  Diwani viti maalumu Murungi Kichwabuta muda mfupi baada ya Nape  kutengua maamuzi ya kufukuzwa kwa madiwani 8 wa ccm akiwa na Diwani wa kata ya Bakoba Felician Bigambo wa CUF
 Diwani wa kata ya Bakoba (CUF) Feliciani Bigambo  akipoongea na wananchi. Amesema wananchi wangewashangaa CCM kuona watetea haki za wananchi ndio wanaonekana  maadui na kukumbatia mafisadi, na kwamba  kama madiwani wanafanya kazi kwa sheria na kanunu za vikao,hivyo watahakikisha haki za wananchi zinapatikana
Katibu mwenezi wa CCM Bukoba mjini Kamadhani Kambuka akieleza kuridhishwa kwake na kauli ya Nape kupitia vyombo vya habari
Diwani wa kata ya Bakoba Felician Bigambo (CUF) akiwaeleza wananchi  kuwa Nape amefanya jambo la msingi kutengua maamuzi ya watu wachache wanaokumbatia mafisadi na kuwakatisha madiwani tamaa wanaodai haki ya wananchi wa Bukoba mjini. Amesema madiwani wanafanya kazi kwa taratibu na sheria na kanuni, hivyo watahakikisha haki inapatikana kwa kushirikiana na madiwani wa CCM  wanaojari kero  na haki za wananchi waliowachagua na sio kikundi cha watu wachache wanaokumbatia mafisadi
Diwani wa kata ya Kashai ambaye pia ni mwenyekiti wa wilaya Bukoba mjini akipongezwa na wananchi muda mfupi baada ya maamuzi ya alimashauri kuu ya ya mkoa kutenguliwa

NAPE ALIPOTANGAZA HATMA YA MADIWANI WANANE WALIOTIMULIWA BUKOBA, KWAMA SASA IKO MIKONONI MWA KAMATI KUU YA CCM


Nape akizungumza na Waandishi leo, Dar es Salaam
HATIMA ya madiwani wanane wa CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, waliovuliwa uongozi na Halmashauri Kuu ya CCM mkoa Kagera, sasa ipo mikononi mwa kamati Kuu ya CCM.

Hatima hiyo, imetangazwa leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo.
Akizungumza na waandishi, Nape amesema kwamba licha ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kutangaza uamuzi wake wa kuwafutia madiwani hao dhamana ya CCM, jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba, CCM Makao Mkuu imewataka madiwani hao kuendelea na kazi kama kawaida wakati wakisubiri maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM ambayo itakutana mjini Dodoma Agosti 23, mwaka huu.
"Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho.  Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe", alisema Nape na kuongeza;
"Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera".
Nape alisema, pia CCM makao makuu wamepokea barua ya madiwani hao kukata rufa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Alisema, wakati sakata hilo likiwa bado lipo katika hali hiyo, CCM inawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.
Akifafanua zaidi Nape amekanusha kwamba, Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete alipokuwa katika ziara ya kiserikali mkoani Kagera, alitumia fursa hiyo pia kuwapatanisha madiwani na Meya katika mgogoro unaodaiwa kuota mizizi baina yao.
Nape amesema, Rais Kikwete aliagiza hatua za kumaliza mgogoro huo zimalizwe kwa kufuata sheria na kanuni kwa lengo la kuhakikisha kuwa hakuna upande utakaoonewa au akupendelewa.
Akitangaza jana  Katibu wa CCM wa mkoa wa Kagera, Avelin Mushi,aliwataja madiwani waliotimuliwa kuwa ni,  Yusuph Ngaiza (Kata Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba, Samwel Ruangisa (Kitendagulo) ambaye ni Meya mstaafu na Mkuu wa mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera, Murungi Kichwabuta (Viti maalumu) Deusdedith Mutakyawa (Nyanga) Richard Gaspal (Miembeni)Alexander Ngalinda (Buhembe) ambaye pia alikuwa Naibu MeyaDauda Kalumuna (Ijuganyondo) na Robert Katunzi wa kata Hamugembe.

Post a Comment

0 Comments