Mbunge Peter Mathuki kutoka Kenya aliyewasilisha hoja binafsi kwenye bunge la EAC leo |
Arusha
Sakata la vikao vya Bunge la Afrika Mashariki kufanyika kwenye
nchi wanachama kwa mzunguko limeingia katika sura mpya baada ya kikao cha Jana jioni kuvunjika kufuatia Spika wa
Bunge hilo,Magreth Zziwa Nantongo kukataa hoja binafsi ya mbunge kutoka Kenya
Peter Mathuki aliyetaka utaratibu wa zamani kufanya vikao kwenda nchi wanachama
uendelee.
Mbunge alimama na kuomba kuwasilisha hoja hiyo ambayo Spika
aliitupilia mbali kuwa haina mashiko na kusababisha wabunge kutoka Rwanda
kutoka nje ukumbi wa bunge yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
Spika alitoa mapumziko na mashauriano ya dakika 15 na
aliporejea wabunge wapatao 14 tu ndio walikubali kuingia ukumbini huku wengine
wakigomea uamuzi wa Spika kukataa hoja ya mbunge kuwasilishwa na kuamua
kuahirisha bunge hadi kesho.
Wabunge wanaounga mkono vikao kufanyika Arusha wanadai kuwa
ni jambo la busara kutokana na kuwa ndio makao makuu ya EAC na fedha nyingi
zimetumika kujenga makao hayo na iwapo vikao vya bunge vitafanyika kwa
kuzunguka nchi wanachama zitatumika fedha nyingi kulipia kumbi za kufanyia
vikao hivyo fedha ambazo zingetumika kwa shughuli za maendeleo.
Kwa upande mwingine wanaotaka vikao vya bunge vifanyike kwa
mzunguko wanajenga hoja kuwa itasaidia kujenga uelewela wa mtangamano kwa
wananchi na taasisi za kiraia kufatilia mwenendo huo kwa karibu.
Mbunge wa Tanzania,Nderakindo Kessy alipotakiwa kutoa maoni
yake alisema jambo hilo limechukua sura mbaya na anayeweza kulizungumzia ni
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Adam Kimbisa ambaye hakuwepo na alipotafutwa
Katibu wake Shyrose Bhanji alikua kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia