Makao
Makuu ya kituo cha habari na mawasiliano cha Redio ya jamii Sengerema
Fm mkoani Mwanza kunakofanyika warsha ya wiki moja kwa redio za jamii
nchini kwa ajili ya kuziandaa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Meneja
wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Radio Sengerema mkoani Mwanza
Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kutoka
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa
Wakurugenzi na Mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya
wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO kupitia mradi wa DEP kwa ajili ya
kuwaanda kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea
uchaguzi wa mwaka 2015.
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumza na mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania nchini katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya mradi wa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
Mshauri
wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo
kwa washiriki wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani
Sengerema mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mradi wa DEP
kutoka UNESCO Courtney Ivins, Afisa Mipango Taifa wa Kitengo
cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin na Mhadhiri wa Chuo
kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr.
Ambrose Kessy.
Meneja
wa Redio Sibuka Fm Maswa Bi. Bhoke Okachu akiwasilisha maoni wakati wa
kujadili mradi wa DEP kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani
Sengerema mkoani Mwanza.
Picha
juu na chini ni Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa
redio za jamii 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaohudhuria warsha
hiyo.