Waziri
wa maji Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wajumbe wapya wa bodi ya
mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)wakati wa hfla fui
ya kuizindua bodi hiyo iliyofanyika katika ukumbu wa bodi wa mamlaka
hiyo.
Mkurugenzi
wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA) Cyprian
Luhemeja akisoma taarifa mbele ya waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe
wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya mamlaka hiyo.
Waziri
wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa
wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)
Hajira Mbande ambaye pia ni meneja wa Azania Bank tawi la Moshi.
Waziri
wa maji Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi kwa mmoja wa
wajumbe wa bodi ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)
cyprian Luhemeja ambaye pia ni mkurugenzi wa MUWSA.
Baadhi
ya wageni pamoja na wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na maji taka
mjini Moshi(MUWSA)wakifuatilia hotuba ya waziri wa maji Profesa Jumanne
Maghembe wakati wa uzinduuzi wa bodi mpya wa mamlaka hiyo.
Wajumbe
wa bodi mpya ya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi
(MUWSA)katika picha ya pamoja na waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi
WAZIRI
wa maji Prof Jumanne Maghembe, amesema mara baada ya notisi ya miezi
sita kumalizika,serikali italazimika kuzikatia maji baadhi ya taasisi
zake likiwamo jeshi la polisi na magereza kutokana na kuwa na
malimbikizo ya deni la Ankara za maji la zaidi ya Sh Bil 5.3 nchini
kote.
Amesema
taasisi hizo zilipewa notisi ya kuhakikikisha zinalipa malimbikizo yao
kwa kipindi cha mwezi April hadi Septemba mwaka huu, lengo likiwa ni
kuhakikisha mamlaka za maji zinazodai fedha hizo zinaweza kuendesha
shughuli zake bila vikwazo vyoyote.
Prof
Maghembe amesema hayo wakati akizindua bodi mpya ya wakurugenzi ya
mamlaka ya majisafi na taka mjini Moshi(MUWSA), yenye wajumbe 10,ingawa
pia alisisitiza umuhimu wa mamlaka za maji kutotanguliza suala la
kuwakatia wateja huduma hiyo bali kuwaelimisha na kabla ya uamuzi wa
kusitisha huduma.
Wajumbe
wa bodi hiyo ni mwenyekiti, Shally Raymond,makamu mwenyekiti Prof
Faustine Bee,katibu Cyprian Luhemeja, wengine ni Japhary
Michael,Elizabeth Minde,Boniface Mariki,Alfred Shayo,Hajira
Mmande,Abdala mkufunzi,Mtoi Kanyawana na Bernadette Kinabo.
“Hizi
taasisi za serikali tunafahamu kwamba zinamadeni makubwa, ipo inayodaiwa
hadi Mil 400, tayari tuliwapa notisi April hadi Septemba mwaka
huu…tumewaeleza msipolipa tutakata huduma, maji ni gharama lazima
yalipiwe ili mamlaka ziboreshe miundombinu yake” alisema Maghembe.
Mapema
katika taarifa yake,mkurugenzi wa MUWSA ambaye pia ni katibu wa
bodi,mhandisi Cyprian Luhemeja alisema mamlaka imejipa siku 180 za
mabadiliko ambapo alimuhakikishia waziri kwamba hadi kufikia Disemba
mwaka huu mamlaka itakuwa imepunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 39
hadi tisa.
Aidha
mkurugenzi huyo alisema katika mpango wa matokeo makubwa sasa ‘Big
result now’ pia wamekusudia kuongeza idadi ya wateja kutoka 21,000 hadi
kufikia 35,000 ifikapo Disemba mwaka huu lengo likiwa ni kufikia wateja
50,000 ifikapo Juni mwaka 2014.
Naye
makamu mwenyekiti wa bodi hiyo,Prof Faustine Bee, alisema bodi
itahakikisha siku 180 zinatoa matokeo yaliyokusudiwa na kutaka
wafanyakazi kutoa ushirikiano kwani miongoni mwa mambo yatakayopewa
kipaumbele ni maslahi yao.