Picha juu na chini ni sehemu ya wafuasi
wa chadema wakitimua mbio leo muda mfupi baada ya jeshi la polisi
mkoani arusha kuwatawanya wakati wafuasi wa chadema walipotaka kuanza
kuaga miili ya watu waliofariki kwenye mlipuko wabomu kwenye mkutano wa
chadema
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amewavua
madaraka maofisa wanne wa polisi kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo, huku
akiwafukuza kazi askari saba wa vyeo vya chini pamoja na kuwapa onyo
wawili kutokana na kushiriki moja kwa moja katika matukio ya wizi,
kusababisha mauaji na uzembe kazini.
Nchimbi alipoulizwa sababu za kutowafukuza kazi
maofisa wa juu, badala yake amekuwa akiwavua madaraka alisema, “Hawa
niliowataja sio kama wanahusika, tunawavua madaraka kwa sababu ya
kushindwa kusimamia majukumu yao kikamilifu. Madaraka waliyopewa
yamewashinda hivyo tumewanyang’anya.”
Maofisa waliovuliwa madaraka ni Mkuu wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha, Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro,
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mvomelo, Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha
Polisi Dumila, Juma Pamba na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kasulu, Daniel
Bendarugaho.
Hii ni mara ya pili kwa Dk Nchimbi kuwachukulia
hatua maofisa wa polisi, kwani Machi mwaka huu waziri huyo aliwafukuza
kazi maofisa watano wa polisi na kumsimamisha kazi kwa mwezi mmoja
Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi hilo, Renatus Chalamila kutokana
na kuhusishwa na rushwa katika kuajiri.
Pia aliwafukuza makuruta 95 waliokuwa Chuo cha Polisi (CCP), Moshi kutokana na kugundulika kutumia rushwa kupata ajira.
Maofisa watatu kati ya hao watano walifukuzwa
kutokana na kugundulika kuwa walikamata dawa za kulevya aina ya cocaine
lakini zilipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ziligundulika ni chumvi
na sukari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk
Nchimbi alisema amechukua hatua hiyo baada ya kupata ripoti ya kamati
aliyoiunda kuchunguza matukio yaliyotokea kati ya Desemba 26 mwaka jana
na Mei 18 mwaka huu.
Alisema matukio hayo ni lile la gari la FFU
kutumika kubeba bangi mkoani Kilimanjaro, polisi kutumia fuvu la kichwa
cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kesi kwa lengo la kupata fedha
mkoani Morogoro pamoja na mauaji ya mfanyabiashara wilayani Kasulu
yaliyofanywa na askari wawili.
Sababu za kuvuliwa madaraka
Alisema Giro amevuliwa madaraka kutokana na
kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maofisa walio chini yake na
kusababisha Mei 18 mwaka huu, kutumika kwa gari la polisi lenye namba za
usajili PT 2025 kubeba bangi kilogramu 540 zenye thamani ya Sh81
milioni.
“Yeye ndiye msimamizi wa magari yote ya FFU na
ndiye mkuu wa kikosi hicho katika mkoa huo, kwa utaratibu wa magari ya
FFU hayaendi popote bila yeye kujua, ikitokea hakujua na mpaka gari
limevuka nje ya mkoa maana yake hakutimiza wajibu wake ipasavyo, kamati
ilishauri avuliwe madaraka,” alisena na kuongeza;
“Nilipoipata taarifa ya kamati juzi niliagiza polisi wamvue madaraka na hilo lilifanyika siku hiyohiyo.”
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia