HAI WAJIPANGA UPYA KATIKA SWALA ZIMA LA USAFI WA MAZINGIRA



NDUGU MGENI RASMI
IFUATAYO NI TAARIFA FUPI KUHUSU KAMPENI YA KITAIFA YA USAFI WA MAZINGIRA              16/08/2013
UTANGULIZI
Wizara  ya Afya  na Ustawi  wa  Jamii inaratibu  utekelezaji  wa  kampeni  ya Kitaifa  ya Usafi  wa  Mazingira  inayoendelea  kutekelezwa  hapa  nchini  katika  Halmashauri  112 .Lengo  la  Kampeni  hii  ni  kuhamasisha  ushiriki  wa  jamii  katika  kuboresha  hali  ya  usafi wa  mazingira  katika  ngazi  ya kaya  na  taasisi ( shule).Inatarajiwa  ifikapo mwaka  2015  jumla  ya  vyoo  bora  vya  kaya  1,520,000  au  zaidi  na  shule  zenye  huduma  bora  ya  usafi  wa  mazingira  802  zipatikane  kutokana  na  kampeni  hii .Msingi  wa  Kampeni  hii  ni  kubadili  tabia  na  mtazamo  wa  jamii katika   kutathimini  suala  la  usafi.
Wizara ya Afya inatekeleza kampeni ya usafi wa mazingira kwenye Halmashauri za wilaya 112, wilaya ya Hai ni miongoni mwa wilaya hizo, kampeni hii ilianza na halimashauri 42 na sasa zimeongezeka  70, kampeni hii imelenga kuleta mabadiliko katika maeneo mawili muhimu ambayo ni ngazi ya kaya na ngazi ya shule za msingi  
Kampeni hii ilizinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5/6/2012 mkoani  Kilimanjaro.

MTAZAMO  WA  KITAIFA
Mheshimiwa mgeni rasmi
Tanzania  imekuwa  ikipambana  kuboresha  afya  na usafi  wa  mazingira .Kampeni  ya  MTU  NI  AFYA  iliongeza  matumizi  ya  vyoo kutoka  asilimia  20%  hadi  kufikia  asilimia  80%  katika  kipindi  cha  miaka  mitano  (1973-1978) .Jitihada  nyingine  ziliendelea kufanyika  na  serikali   kwa  kuhusisha  HESAWA,  PHAST  pamoja  na mradi  wa  Maji  (WSP) ambazo zilisaidia  kuongeza  usafi    wa  mazingira  na  kujenga  vyoo  vya  gharama  nafuu. Jitihada  hizi  zilipelekea  jamii  kuacha  kunya  ovyo   Baadhi  ya  tafiti  zilionyesha  kuwa  kaya  nyingi  zilikuwa  na  vyoo  ambavyo  havijaboreshwa au  wanavyo  vya  kienyeji.  Tanzania  kama  nchi  nyingine  yoyote  inayoendelea  haikuwa  nyuma  kwenye  swala  la  utunzaji  wa  mazingira  kwa  kupunguza idadi  ya  watu   wasiokuwa  na  vyoo  .Jitihada  kubwa  sasa inafanyika   kuboresha  vyoo  vilivyopo. 
 Jamii inatakiwa   ishirikishwe  kikamilifu  ili  waweze  kuamua  nini  kifanyike  katika kuboresha  mazingira  .Mbinu  inayoleta   mafanikio    haraka  ni  vema  ikatumika,   hivyo  katika  usafi wa  mazingira  mbinu  ya( CLTS COMMUNITY LED  TOTAL  SANITATION)ushiriki   wa  jamii  katika  kuboresha  mazingira  imependekezwa  itumike  kuhamasisha  maswala  ya  afya  na usafi  wa  mazingira  nchini,  chini  ya  Kampeni  ya  usafi  wa  mazingira  kitaifa.

Mbinu  hii  ya  ushiriki wa jamii  katika  kuboresha  hali   ya usafi  wa mazingira     ( CLTS)   ilitambulishwa  nchini  Tanzania mwaka2007 na  PLAN  INTERNATIONAL  kwa kuanzia   Mkoa  wa  Pwani  ( Kibaha na  Kisarawe  ) na  Mwanza (Geita )  na  baadaye  wakaendelea  kwenye  Halmashauri  10  ambazo  ni Sumbawanga,Iringa , Masasi ,Rufiji  Kiteto  ,Mpwapwa, Kondoa ,Igunga,Karagwe  na Musoma.  Tathmini  iliyofanywa  na ( WSP)  Program  ya  maji  na  usafi  wa  mazingira  katika Halmashauri  10 mwaka  2012  zilibaini  zaidi  ya  vitongoji  133  ambayo ni  80%  kati  ya  vitongoji  166   sawa  na asilimia  50%  waliahidi  kuacha  kunya  hovyo  .Pamoja  na  ahadi , jitihada  zaidi  zinatakiwa   zifanyike  ili  kuendelea  kuboresha  usafi  wa mazingira.
Wizara  ya  Afya  na Ustawi wa  Jamii  katika kipindi hiki inatekeleza  kampeni ya  Mazingira   na Ushiriki  wa  jamii  katika  kuboresha  hali  ya usafi  wa  mazingira . Mbinu  iliyopendekezwa  itumike  kuishirikisha  jamii  wakati  wa  kampeni  kwani  ni  rahisi  kutekeleza  ina  gharama   nafuu   na  rasilimali  zinazotumika  zinapatikana  kwa  urahisi . Mpaka  kufikia  kipindi  hiki  Halmashauri  chache  ndio  zina wawezeshaji  wachache   waliopatiwa  mafunzo  ya mbinu  hii  .Hivyo  Wizara  ya  Afya  na  Ustawi   wa  jamii  imeamua  utaratibu  huu  utumike  nchi  nzima  kwa  kutoa  mwongozo  utakaotumika na wawezeshaji  wote  katika  utekelezaji  wa   usafi  wa  mazingira .      Mbinu  ya    ushiriki  wa  jamii  katika  kuboresha  hali  ya  usafi  wa   mazingira  (CLTS)  inasababisha  jamii   ichukue  hatua  za  haraka  kutokana  matokeo  yanayoonekana  baada  ya  kuwezeshwa  kwa kuanza  kuchimba  vyoo   kwa  gharama  nafuu  na  kuvitumia  pamoja  na  kufanya  ukarabati  wa  vilivyopo  ili  viweze  kutumika  .Pia  kwa  kuogopa  kula  mavi   ya  wengine   jamii     inaweza   ikaanza  kumsaidia  yule  asiye  na  choo kwa  kumjengea  choo  ili  atumie  au  waruhusiwe  wasio  na  vyoo  kutumia  vyoo  vya  wengine  ili   jamii  ipate  uhakika  wa  asilimia  100%   kwamba  hakuna ambaye  atakunya  hovyo  au  atakaye  kula mavi  ya  mwingine.

LENGO LA KAMPENI :
Mheshimiwa mgeni rasmi lengo la kampeni hii ni:
-Ujenzi wa vyoo bora na matumizi yake
-Unawaji wa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka
-Uchimbaji wa mashimo ya taka na matumizi ya vichanja.

Mbinu itakayo tumika katika kampeni hii inaitwa  CLTS (COMMUNITY LED TOTAL SANITATION) yaani ushiriki wa jamii katika kuboresha hali ya usafi wa mazingira.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post