HALMASHAURI YATOA ZABUNI KWA MTU ASIEKUWA NA OFISI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Halmashauri ya Meru mkoa wa
Arusha imetoa zabuni kwa mkandarasi ambaye hana ofisi wala makazi maalumu kwa
ajili ya kufanya na kubuni kazi mbalimbali ndani ya jamii ikiwemo
miradi ya maji katika baadhi ya Vijiji hali
ambayo imesababisha halmashauri hiyo kukosa miradi ya maji mpaka sasa.

Hayo yameebainika mara baada yaNaibu waziri wa maji Bilith
Mahenge kutembelea baadhi ya miradi  ambayo
ipo chini ya Halmashauri mapema jana(leo) ambapo inadaiwa kuwa Halmashauri hiyo
ni moja ya Halmashauri yenye Vyanzo vingi vya maji lakini haina maji

Akisoma taarifa hiyo mhandisi wa maji kwenye wilaya hiyo
Maningo Mohamed alidai kuwa kwa kipindi cha mwaka 2010 mpaka April Mwaka jana
mkandarasi kutoka katika kampuni ya free World  Co Ltd aliingia
mkataba na halmashauri hiyo kwa malengo ya kufanya kazi
lakini hakuweza  kufanya kazi hiyo na
badala yake alikuwa anatoa visingizio vikiwemo vya kucheleweshea bajeti ya
Serikali kwenye sekta ya maji.

Mhandisi Mohamed alidai kuwa mara baada ya kupewa mkataba
mkandarasi huyo alisumbua sana halmashaurikwa kuwa hakuwa na vifaa lakini pia
hata ofisi hali ambayo iliendelea kukwamisha miradi ya maji katika Wilaya hiyo
hivyo kusababisha madhara makubwa ya uhaba wa maji

“hii kampuni ilipewa mkataba lakini kwa bahati mbaya
waliodanganya kuwa wana ofisi baada ya kuwafuatilia kwa undani tuliweza kujua
na kutambua kuwa hana uwezo lakini tulishindwa kumuondoa kutokana na sheria juu
ya makandarasi zinavyobana”aliongeza Mhandisi huyo.

Aliongeza kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imesababisha madhara
kwa kuwa malengo hasa kwenye sekta ya maji bado hayajafikiwa na badala yake
hata kiwango cha maji ambacho kinazalishwa bado nacho hakiwezi kuwatosheleza
wananchi,

Akiongelea uhaba wa maji katika Wilaya hiyo alidai kuwa
suala la uhaba wa maji linaendelea kukua kwani kwa sasa lita zinazoitajika ni
lita za ujazo elfu kumi na tano mia tano wakati zinazoaalishwa ni lita elfu
sita tu kwa siku jambo ambalo linasababisha uhaba mkubwa wa maji.
Mhandisi Mohamed alibainisha kuwa uhaba huo wa maji
unasababisha madhara makubwa sana kwani wananchi wa wilaya hiyo wanalazimika
kutembea umbali mrefu sana kwa ajili ya kutafuta maji huku shuguli za kila siku
zikiwa zinakwama

Awali Naibu Waziri wa maji Dkt binilith Mahenge alidai kuwa
sakata la mkandarasi ambaye hana ofisi wala vifaa ni sakata la kuhudhunisha
sana kwani huo ni uzembe wa baadhi ya watendaji wa Halmashauri hiyo kushindwa
kuwakagua wakandarasi kabla ya kuwapa mikataba ya kazi.

Dkt Mahenge alisema kuwa sakata hilo linatakiwa kuwa la
kwanza na la mwisho na uongozi wa Halmashauri unatakiwa kuomba hata msaada kwa
makandarasi wakorofi kwani wanasababisha hata miradi ya Halmashauri ikiwemo
Maji kukwama.

Aliwataka hata viongozi wa Halmashauri nao kuhakikisha kuwa
wanatafuta mbinu mbalimbali za kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maji kwani
huduma ya maji iliopo bado haiwatoshelezi kabisa wananchi ingawaje wilaya hiyo
ni moja ya wilaya hapa nchini yenye vyanzo vya kutosha vya maji.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post