BREAKING NEWS

Friday, August 23, 2013

BILALI AWAOMBA WADAU WA MIPANGO MIJI EAC KUSAIDIA TANZANIA




Makamo wa kwanza wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal amewataka wadau wa maendeleo wa jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia jitihada za kukabiliana na tatizo la ujenzi holela wa makazi ya watu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maendelo ya makazi  katika jumuiya ya afrika mashariki juu ya upangiliwaji wa makazi katika ukanda wa afrika,ambapo amesema athari za upangiliwaji wa makazi ya watu ni kubwa na linapaswa kuangaliwa kwa karibu zaidi.
Aliongeza kuwa athari za ujenzi holela wa miji na makazi ziko wazi na zinajulikana na kwamba kinachotakiwa ni juu ya namna ya nchi za afrika kuamua kujipanga kulikabili tatizo hilo kwani ni kubwa na kusema kuwa maendeleo ya nchi yeyote yanatokana na upangiliaji wa miji katika sehemu hizo.
Aliwataka pia kuhakikisha wanatoka na kauli moja ya kuhakikisha wanaenda kuwa wabunifu wa kupanga miji yao ili kuweza kuletea nchi za kiafrika maendeleo yanayostahili kwani nchi nyingi za afrika ni masikini kutokana na ujenzi holela wa makazi yao.
Kwa upande wa waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Bi Anna Tibaijuka,amesema kuwa suala la ujenzi holela kwa upande wa Tanzania ni mkubwa na unapaswa kutolewa maamuzi magumu ili kuweza kufanya mabadiliko makubwa ya ujenzi huo .
Alisema kuwa ujenzi holela una madhara mengi ikiwemo kutokuwepo na uwekezaji ambao unateremka thamani siku hadi siku ambapo amesema wanapaswa kubadilisha hali hiyo na kutunza mazingira ili yaendane na wakati pamoja na ujenzi wenye kiwango.
Tibaijuka alisema kuwa kama watanzania wataamka katika nchi yao na kuamua kutengeneza mji wao ni wazi kabisa kutakuwa na maendeleo makubwa na hata wawekezaji watavutiwa zaidi kuja kuwekeza na kusema kuwa kwa pamoja mkutano huo unapaswa kuleta mabadiliko makubwa sana kwani kila mmoja anapaswa kutoa mchango wake ili kuwa na mabadiliko.
Naye mwenyekiti wa kamati ya bunge mazingira na maliasili James Lembeli ambaye pia ni mbunge wa Kahama,amesema kuwa asilimia 80 ya nchi ya Tanzania mji wake haujapangiliwa na kwamba suala la rushwa pia limekuwa ni tatizo la upangaji wa miji sambamba na mazingira.
Akatolea mfano wa nyumba ya kigogo mmoja wa bunge kujenga mita chache na usawa wa bahari hali ambayo inasababisha uharibifu wa mazingira huku walala hoi wanao zunguka eneo hilo wakivunjiwa nyumba zao ambapo nyumba ya kigogo huyo kuendelea kuwepo hali hiyo inaonyesha kuwa sheria ya ardhi na mazingira imekiukwa.
Aliongeza kuwa maeneo mengi yamekuwa na ujenzi wa makazi holela ambapo hali hiyo inaleta ugumu wa kupata huduma muhimu kama vile maji,afya,umeme,pamoja na mambo mengine.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates