Mkuu wa kituo cha polisi
Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa,
akisalimiana na Abdulhalim Humudi, wakati akiikagua timu ya Simba ilipocheza juzi
na timu ya Tanzanite FC, baada ya kutembelea machimbo ya madini ya Tanzanite
Timu ya soka
ya Simba SC ya Jijini Dar es salaam jana imetembelea machimbo ya madini ya
Tanzanite ambapo hapa duniani yanapatikana peke yake Mji mdogo wa Mirerani,
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wachezaji hao
wakiongozwa na viongozi wao Makamu Mwenyekiti, Joseph Itangire (Mzee Kinesi) na
kocha mkuu Abdalah Kibadeni, walitembelea kampuni ya TanzaniteOne na kujionea
namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika.
Hata hivyo,
wachezaji hao wakizungumza kwenye machimbo hayo ya madini ya Tanzanite, walisema
hiyo ni mara yao ya kwanza kutembelea machimbo hayo kwani awali walikuwa
wanasikia Tanzanite katika vyombo vya habari pekee.
Walipotembelea
machimbo hayo pia walicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tanzanite FC
inayomilikwa na Jofrey Nyigu (Mnyalu) na wakaifunga bao 1-0 lililotiwa kimiani
na mshambuliaji wao hatari Abdalah Seseme.
Seseme
alifunga bao hilo baada ya kupewa pasi na Ramadhan Singano “Messi” aliyewachambua
mabeki wa Tanzanite FC, Elibariki Bryson na Abdilahi Yusuph walioshindwa kumpa
ulinzi kipa wao Achibald Kileo.
Baada ya
kumalizika mchezo huo wa kirafiki, timu ya Simba ilikwenda kwenye saluni ya
kisasa ya Nick Baber shop iliyopo Mirerani na kufanyiwa huduma ya kuchuliwa
misuli, kuoga, kusuguliwa uso,miguu na kunyolewa nywele.