BREAKING NEWS

Friday, August 23, 2013

MH. SILAA ATOA SOMO KWA VIJANA JINSI WANAVYOWEZA KUISHI NDOTO ZAO

20130818_161729_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga wakati alipofika kwenye chimbo hilo kuzungumza na vijana baada ya kuitikia mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti huyo.
20130818_162938_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwenyekiti wa Chimbo School of Thought ambaye pia ni mtangazaji wa redio Clouds na TV Harris Kapiga.
20130818_164446_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akitema cheche kwa vijana na kuwatia moyo.
20130818_175056_resized
Mmoja wa vijana akimuuliza maswali Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Na.Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa katika ya nchi ya Ahadi Sinza Kamanyola amefunguka kuhusiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto zake.
Moja ya mambo aliyoyazungumzia ni pamoja na kijana kujitambua na kujua nini hasa anataka na anapata vipi kwa maandalizi ya kutimiza nia yake.
Mh. Jerry pia amechambua mada hiyo kwa marefu na vijana kuonekana kumuelewa ipasavyo na hivyo kubaki kazi kwao kutekeleza na kuyafanyia kazi yale aliyoyazungumza, ikiwemo kujua lengo lao hasa ni nini na kujipima wanautayari wa kiasi gani katika kutekeleza hilo lengo na kubwa zaidi ni uthubutu wa kufanya jambo lenyewe.
Katika mazungumzo yake kilichowavutia vijana wengi zaidi ni pale alipowaeleza kuwa yeye Mstahiki alithubutu kugombea udiwani ndani ya kata ya Ukonga akiwa na umri wa miaka 23 na kufanikiwa kushinda.
Ni jambo la kujivujia kuwa na vijana hasa kama mstahiki Jerry Silaa ambaye pamoja na kuwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya Chama tawala cha CCM Taifa.
Pamoja na hayo Mh. Jerry Silaa amewaeleza vijana kutambua hizo ndoto ni za nani hasa na ni nani wakuzifanikisha kama si wenyewe.
Aidha, zaidi ya hapo amewaasa vijana kuwa na majibu ama matokeo ya kila wanalofanyia kazi "being result oriented" na kupata kile wanachokitaka kwa kuzingatia lengo pamoja na muda kiutendaji.
20130818_183833_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza kumsikiliza wakati akifunguka kuhusuiana na namna gani kijana anaweza kuishi ndoto yake.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates