BREAKING NEWS

Monday, August 19, 2013

HII NI AIBU GANI KATIKA RIADHA TANZANIA



Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akiwa Moscow


Wakati nchi za ulimwengu zikiwakilishwa na wanariadha wake mahiri katika mashindano ya dunia ya riadha mjini Moscow Urusi, Tanzania imevunja rekodi ya aina yake kwa viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania kutangulia Moscow huku wakiwaacha wanariadha nyuma.

Rais wa RT (aliyechaguliwa kinyume na katiba) bila wasiwasi, aibu wala uzalendo amekwenda Moscow wiki iliyopita huku walengwa wenyewe wa mashindano ya (World Athletic Championships) ambao ni wanariadha wanaotegemewa kupeperusha bendera ya Tanzania na kupigania medali wakibaki nyuma.
Cha ajabu zaidi ni pale ambapo kiongozi huyo wa RT alipofuatana na kiongozi wa zamani wa chama hicho kwa kile kinachodaiwa hana uzoefu katika mikutano ya Chama Cha Riadha duniani (IAAF), kitu ambacho kinafanywa kuwa kisingizio cha viongozi hao kutangulia.

Kimsingi kiongozi huyo wa zamani alikusudiwa kuwa kama kocha mwandamizi atakayefuatana na wachezaji, ila sasa imekuwa sawa na rubani kuwaacha abiria nyuma. Sijawahi kusikia kocha wa Taifa Stars akitangulia wiki moja kabla kwenye viwanja vya matukio bila kuongozana na wachezaji wake, lakini kwa sababu RT ni mali ya TOC hakuna cha kushangaza hadi hapo, watanzania waendelee kutafakari kwa kina tabia hiyo mbaya inaendekezwa na nani, na kwa masilahi ya nani?.

Je inawezekana kwamba rais huyo mtata wa RT anazungukwa na wajanja waliokwishaonja utamu wa fedha za makampuni yaliyowahi kutudhamini?, nikimaanisha huenda kuna mpango unasukwa wa kuitapeli makampuni kama ilivyokuwa PUMA na LINING?. Ili kiongozi huyo wa RT mgeni asiyeelewa ‘umafya’ wa viongozi wa sasa na wa zamani wa TOC wenye ushawishi mkubwa RT kutumika tu kama chambo (cheo) ili wajanja wale ‘sinia kubwa’ wakati kiongozi mpya akifurahia posho (per day) huku taifa likiendelea kupoteza sifa katika viwanja vya mchezo wa riadha, ‘masikini taifa limetelekezwa na wahusika’. Ambao wangechunguza kiini cha matatizo ya TOC na RT taifa lingekombolewa.

BMT na wizara inayohusika na michezo inastahili kuwa na hisia ya maumivu pale Tanzania inapojikuta nyuma kila wakati panapotokea mashindano ya kimataifa, swali muhimu ni; Je wahusika wa TOC na RT wanalindwa na nani?, na ulinzi huo ni kwa masilahi ya nani?, na ulinzi huo utaendelea hadi lini?.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates