BABU TALE ASEMA YUKO TAYARI KUMPOKEA DOGO JANJA TIP TOP HATA LEO.....JANJARO ASEMA NIPO TAYARI KWA MAELEWANO NA MADEE NAYE ASEMA AMEMSAMEHE DOGO JANJA ZAMANI


BOB TALE


Imeonekana kama drama flani hivi na kuchukuliwa kama Story ya kimya kimya flani hivi ila kwa sasa imekuwa wazo kupitia DJ HAAZU wa MJ Radio ARUSHA ambaye ameamua kuziunganisha sauti za Vichwa Vitatu ambavyo ni Janjaro, madee na Bob Tale.

JANJARO NA MADEE
Ni juzi juzi tu ambapo Manager wa kundi la TipTop Connection Bob Tale alifunguka kuwa Dogo Janja anampigia magoti Madee kuwa wamrudishe TipTop na hapa ikabidi Haazu apate sauti za Wahusika wote kupitia MJ RADIO ambapo alimpigia simu Bob Tale ambaye alithibitisha hilo na kuonekana wazi kuwa anatamani Dogo janja Arudi TipTop Connection huku akijilinda na kile alichokiita kuwa yeye na Janjaro zinaiva na hajawahi kugombana na Dogo janja.

Msikilize Bob Tale hapa chini akimthibitishia Haazu kuwa yuko tayari Dogo janja arudi TipTop
DJ HAAZU alipotamani kujua kutoka kwa Tale kuwa labda alijisikia vibaya kipindi ambacho Dogo alitoka TipTop yeye Tale alijibu kuwa hakujiskia Vibaya kwani ni Maisha aliyokuwa ameamua Dogo ila ukweli umesimama.
msikilize Tale hapo chini tena....
Kwa upande wa story za kitaa zinazodai kuwa Manager wa Mtanashati ent....Ostaadhi juma Namusoma amefulia bado hatujazithibitisha Ila kwa Upande wa Bob Tale alipoulizwa kuwa Janjaro alibug kwenda Mtanashati alijibu kama anauma anapuliza......
Msikilize Tena tale hapo Chini.
DOGO JANJA YEYE ANASEMA BADO YUKO MTANASHATI
Kingine hawezi kubishana na bob Tale

MSIKIZE JANJARO HAPA CHINI
LAKINI JE KUHUSU JANJARO YUKO TAYARI KURUDI TIPTOP?????

Hilo ndilo lilikuwa swali la pili la DJ HAAZU kwa Dogo Janja ambapo yeye alijibu kuwa yuko tayari kurudi ila kwa Maelewano ya maana kuhusu kulindiwa na kupewa haki yake inavyostahili na sio mapichapicha.
Msikilize Janjaro hapo chini akifunguka
DOGO JANJA ANAJUA OSTAADHI KAFULIA?
Hili lilimuhusu pia janjaro ambapo yeye alijibu kuwa kuna wakati mtu anayumba kiac flani ila hawezi Msemea Ostaadhi kwani atakuwa anaingilia Uhuru wa mtu Binafsi.

Msikilize tena hapa Janjaro akifunguka kuhusu Kesi ya kuwa Boss wake Kafua
JE MADEE YEYE ANASEMAJE...?
DJ HAAZU akataka kujua kama Raisi wa TIpTop Madee ambaye yeye ndiye aliyekuwa ametajwa na Janjaro kama mhalifu wake wakati anatoka TipTop Je atakuwa ameyamaliza na janjaro?, ambapo Madee yeye amesema alishamsamehe Dogo kitambo sana na akamwambia kabisa kuwa amemsamehe na kwamba wanaongeaga na Janjaro kama Mdogo wake na kusema kuwa alijua ni watu waliokuwa wanataka kumuharibia future janjaro ila kwa sasa ukweli umesimama na yeye toka kipindi kile alimchukulia Dogo kama mtoto na ndio maana akatekwa  kirahisi ila kwa sasa Dogo Kajua ukweli na yeye Madee kuthibitisha kuwa hakumlaumu Dogo
MSIKILIZE MADEE HAPO CHINI AKIFUNGUKA MADEE AMESHAMWAMBIA JANJARO KUWA AMEMSAMEHE MSIKIE TENA HAPO CHINI HIYO NDO HABARI KAMILI KWA SASA KAMA OSTAADHI KAFULIA KWELI BASI ENDELEA KUFUATILIA STORY ZETU HAPA HAPA.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post