Timu nzima ya utafi ikiwa jijini Mwanza
Jumuiya
ya Afrika Mashariki(EAC)kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la
Ujerumani(GIZ) imemaliza awamu ya kwanza ya utafiti wa uelewa wa
wananchi juu ya jumuiya hiyo.
Hapa nchini zoezi la kuwahoji
wananchi limefanyika katika mikoa ya Dodoma,Mwanza,Mara na
Unguja-Zanzibar ambapo idadi iliyokusudiwa ilifikiwa kwa kujibu maswali
yaliyoandaliwa kwenye dodoso na wao kutoa mapendekezo jinsi ambavyo
wanadhani ni njia bora ya kuhakikisha wananchi wa Jumuiya hii
wananufaika.
Baadhi ya wananchi walionesha kutokuelewa mambo
mengi na kutaka elimu zaidi itolewe na EAC kwa kushirikiana na wizara ya
Afrika Mashariki kwa upande mwingine.
Utafiti huo pia umefanyika katika nchi wanachama wa EAC ambao ni Kenya,Tanzania,Rwanda na Burundi |