KITITA cha sh. milioni 100 kitatumika kugharamia shughuli ya mazishi na msiba wa mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, aliyeuawa juzi kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Tajiri huyo Erasto Msuya ambaye ni ambaye ni mtoto wa pili kati ya saba wa Elisaria Msuya maarufu kwa jina la Kikaango alipigwa risasi zaidi ya kumi, na watu wasiojulikana katika eneo la Mjohoroni, katikati ya mji wa Bomang’ombe na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimajaro (KIA), alipokuwa akisafiri kutoka Moshi kwenda Arusha, juzi mchana.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya mazishi aliyezungumza na theNkoromo Blog, kwa sharti la kutotajwa jina, amesema kiasi hicho fedha kitaghramia kununua jeneza na kukodisha gari maalum ya kubeba mwili kutoka jijini Arusha kwenda Mirarani, wilayani Simnajiro ambako mazishi yamepangwa kufanyika Jumanne ijayo.
Amesema, jeneza na gari la kubeba mwili tayari vimeagizwa jijini Nairobi, Kenya kwa gharama ya sh. nane na kufafanua kwamba wamelazimika kukodisha gari maalum ya kubeba maiti kutoka Nairobi kwa kuwa barabara ya kwenda Mererani kuwa mbaya kiasi cha kuhitaji gari lenye uwezo mkubwa tofauti yanayopatikana jijini Arusha ambayo mengi ni madogo.
Kamati ya maandalizi ya mazishi hayo inaongozwa na Gady Msuya, kaka mkubwa marehemu na leo wajumbe walikuwa wakikutana kwa vikao nyumbani kwa mareehemu eneo la Kwa Idd, nje kidogo ya jiji la Arusha kukamilisha mipango ya mazishi hayo huku waombolezaji wanaomiminika nyumbani kwa marehemu wakikirimiwa kwa vyakula na vinywaji wahudumu wakiwa ni maalum kutoka hotel ya SG Resort inayomilikiwa na marehemu Msuya.
Kifo cha tajiri huyo, kimeacha utata miongoni mwa wafanyabiashara wenzake ambao wengi wanaendelea kuhoji kwanini mwenzao ameuawa kwa kupigwa risasi nyingi kiasi hicho na watu ambao hawakuondoka wala kupora mali yoyote?