UCHELEWESHAJI WA FEDHA ZA MIRADI INAKWAMISHA KUKAMILIKA MIRADI KWA WAKATI


ucheleshwaji wa  bajeti na bajeti  ndogo inayotolewa na serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya huduma ya maji isiyolingana na gharama ya miradi hiyo imekuwa changamoto ya kutekeleza upatikanaji wa maji katika wilaya ya monduli mkoani Arusha.



Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa halmashauri ya monduli Twalib Mbasha wakati alipokuwa aakisoma taarifa ya maji na changamoto zinzoikuta halmashauri hiyo mbele ya naibu waziri wa maji katika ziara ya utekelezaji wa huduma ya maji pamoja na changamoto zake katika mpango wa vijiji kumi katika wilaya ya arusha.



Aidha mbasha amesema kuwa wamekwa wakitumiwa bujeti ndogo ya na izara ambayo inakuwa tofutti na miradi iliyobuniwa hali ambay wamekuwa wakishinda kutekeleza baaduatia bajeti hiyo kuwa ndogo wananchi wankabiliana na changanamoto ya  upungufu wa maji na hii ni kutokana na ucheleweshaji wa fedha za kuendesheea miradi hii



Pamoja na hayo Mkuu wa wilaya ya monduli Jowika Kasunga amemuhakikishia naibu waziri wa maji DKta Bilinith Mahenge  kuwa miradi iliyoidhinishwa na serikali utekelezaji umeanza na matokeo ya haraka tayari yameanza kuonekana



Akizungumza katika ziara ya ukaguzi wa maradi wa maji katika mamlaka ndogo monduli mkoani Arusha  Kasingwa amesema kuwa mamlaka yake imejipanga vekma katika kuhakikisha tatizo la maji mjini na vijijini linatatulika japo hata kwa sasa hakuna tatizo la maji kwa wananchi wake.



Aidha Mkuu wa wilaya hiyo wakati akiwasilisha mada zake katika ziara hiyo juu ya michanganuo ya miradi amesema kuwa wilaya ya monduli pamoja  na kuwa na km za mraba 6419 ongezeko la watu pia limeongezeka kwa asilimia 3.9%  ambapo wilaya pia imesema kuwa vituo vya kuchotea maji tiyari mkataba imesainiwa miradi ya vijjii imeanza kutekelezwa,



Vilevile katika suala zima la maji mkuu wa wilaya ya monduli amesema kuwa wananchi kwa asilimia 58.4 ya wananchi ndio  wanaopata maji,na katika halmashauri hiyo utekelezaji kwa mradi wa vijiji kumi ni pamoja na vijij vilivyopewa kipaumbele ni Emaite Eluai, Lolkisale, Lepurko ,Mbaash Emairete Engaruka juu,Lolkisale  Nakerani pamoja na Mbuyuni,



Hali kadhalika mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa hatua za kutatua changamoto hiyo zimenza ambapo ni pamoja na kufufua kijiko na lori kwa makusudi ya uchimbaji malambo.kubuni na kupanua wigo wa mapato ,uhamasishaji jamii katika kushiriki na kuchangia gharama za ujenzi.



Naye naibu waziri wa maji alisema kuwa amesikia chamoto hiyo ya bajeti ndogo ya maji wanayopangiwa ala aliwataka kutumia hela ambayo wanayo mpaka pale itakapoishia ndipo wizara iwaangalie jinsi ya kuwasaidia sehemu ambayo wameishia.



wakati huo huo naibu waziri huyo akiongea na wananchi aliwasihi kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja kulima mbali na maeneo ya vyanzo vyamaji pamoja na kufugammifugo yao mbali na maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na kulinda miundo mbinu ya maji.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post