Msanii Muigizaji wa filamu na
muziki wa bongofleva,Shilole pichani shoto akiimba mbele ya maelfu ya
wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti
fiesta 2013,ndani ya Singida Motel.
Sehemu ya umati wa watu wakishangilia burudani iliyokuwa ikiendelea kwenye kiota hicho cha Singida Motel.
Mkongwe wa muziki wa kizazi
kipya,Sir Juma Nature akiwa na wasanii wenzake wa kundi la TMK -Wanaume
Halisi,wakilishambulia jukwaa vilivyo.
Mashabiki waliokuwa wamejibanza
ubavuni mwa jukwaa,nao walikuwa wakipata ile kitu roho inapenda kutoka
kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
Chumaaaa a.k.a Chid Benz akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
Anajiita mzee wa Mahaba kutoka
Manzabay,Cassim Mganga akiimba nyimbo zake za mahaba,mbele ya maelfu ya
wakazi wa singida na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha hilo
ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Ommy Dimpo a.k.a pozi kwa pozi akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani
Kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa
Dj Mahiri kutoka Clouds FM,Dj
Zero akifinya finya mashine zake kwa namna ya pekee kabisa,iliyokuwa
ikiwafanya mashabiki kibao wazidi kuchenguka na kupiga mayowe kila
wakati.
Wenywewe wanajiita
Makomando,wakilishambulia jukwaani kwa pamoja usiku huu wakati tamasha
la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea ndani ya Singida Motel.
Ni full kujiachia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,wengine wakiwa juu ya miti aaahhh nomaa sanaaa.!
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa
Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya Singida Motel
usiku huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
Petter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku
huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 linaloendelea hivi sasa
ndani ya Singida Motel.
Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea hivi sasa