Ticker

6/recent/ticker-posts

MIUNDO MBINU YA VISIMA KUBORESHWA


SERIKALI imesema kuwa itaboresha miundombinu ya Visima vya maji hasa katika
maeneo ambayo yana visima lakini vinashindwa kutumika kutokana na ubovu
pamoja na uchakavu wa miundombinu ya visima hivyo



Aidha miundombinu ikishaboreshwa itasaidia kwa kiwango kikubwa sana kuweza
kupunguza tatizo la uhaba wa maji hasa maeneo ya  vijijini na hivyo kuweza
kuongeza uzalishaji katika sekta zote ndani ya jamii



Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Maji DktBillinith Mahenge wakati
akiongea na wadau wa maji katika Halmashauri ya Monduli mapema jana
(leo)ambapo alidia kuwa mpango huo kwa sasa upo kwenye maandalizi ya hatua
za mwisho na utaanza hivi karibuni



Dkt Billinith alisema kuwa,katika Nchi ya Tanzania kuna visima vingi sana
ambavyo kama vingeweza kutumika ipasavyo basi vingechangia tatizo la uhaba
wa maji kupungua lakini mpaka sasa baadhi ya visima vinashindwa kutumika
kutokana na ubovu wa miundombinu



Alifafanua kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
miundombinu yote ya visima vya maji itaboreshwa na visima vyote
vilivyojengwa kwa makusudio ya kuwasaidia wananchi viweze kutumika ili
kufikisha malengo ndani ya jamii



“tunataka kila kisima kilichowekwa kwa makusudio ya kuwasaidia wananchi
kiweze kutumika na kusiwe na utaratibu wa kuchimba kisima kama mazoea uweze
kuisha kwani unafanya malengo yua kupambana na uhaba wa maji uweze kuisha
kabisa hapa nchini”aliongeza dkt Billinith

Katika hatua nyingine aliitaka halmashauri ijiwekee utaratibu wa kutafuta
na kubuni vyanzo vya mapato hasa kwenye sekta ya maji ili kuweza kuraisisha
shuguli za maji kwani bado Wilaya hiyo inakabiliwa na matatizo ya uhaba wa
maji

Katika hatua nyingine mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Monduli,Twalibu
Mbasha alidai kuwa pamoja na kuwa wamejitaidi huduma za maji kuwafikia
wananchi wengi wa wilaya hiyo lakini bado kityengo cha maji hakina wataalamu
wa  kutosha

Mbasha alisema kuwa idadi ya wataalamu waliopo kwenye sekta ya maji  ni
wachache  sana huku pia baadhi ya huduma za Halmashauri kukwama hivyo basi
Serikali inatakiwa kuongeza idadi ya wataalamu ili huduma hiyo ya Maji
iweze kuwafikia wananchi wote.

Post a Comment

0 Comments