PICHA YA BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YA KITAMBI NOMA
BAA |
Timu
ya Mwanza Vetereani iliyoshuka jana jioni dimba la CCM Kirumba
kumenyanana Mabingwa wa Ligi daraja la tatu wilaya ya Rorya mkoani Mara
ambapo Rorya walishinda kwa bao 5-1. |
|
Mabingwa
wa ligi daraja la tatu wilaya ya Rorya katika picha ya pamoja na
mfadhili wao mbunge wa Rorya Lameck Airo wa tatu kutoka kushoto
waliosimama nyuma. |
|
Wachezaji
wa Mwanza veterani wakifuatilia mchezo wao na timu ya Rorya ambayo
wameutumia mchezo huo kama kipimo cha maandalizi dhidi ya Kitambi noma
ya Arusha mchezo utakaochezwa siku ya ijumaa dimba la CCM Kirumba. |
|
Safu
ya wachezaji na viongozi wa Mabingwa wa ligi daraja la tatu wilaya ya
Rorya mkoani Mara ikifuatilia mchezo huo ambao timu hii iliibuka
washindi kwa bao 5-1. |
|
Wadau
walioambatana na mfadhili wa timu ya Rorya Sports Club, Mbunge wa Rorya
Mhe. Lameck Airo (kushoto) wakifuatilia hatua za mchezo huo wa kuvutia
uliofanyika jana dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza. |
|
Mashabiki jukwaa kuu. |
|
"Ziara
ya Rorya Sports Club imelenga kuwajengea uwezo wachezaji kucheza
viwanja vyenye ubora zaidi pamoja na kuwafungulia fursa ya ajira kwa
vipaji vyao kuonekana mikoa mbalimbali kanda ya ziwa ili wapate timu
kubwa kusajiliwa na hata kuitumikia timu ya taifa, kwani naamini jimbo
langu lina vipaji vizuri ila havijapata mwanga tu wa wapi pa kuanzia,
ninaamini wakazi wa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera na Tabora
wataamini hiki ninachosema pindi watakapo washuhudia vijana wangu"
Alisema Lameck Airo |
|
Kisha Rorya Sport Club ilishiriki chakula cha jioni na mbunge wao katika hoteli ya Lakairo Kirumba jijini Mwanza. |
|
Kula na kuchati kimtindo. |
|
Chakula cha jioni at Lakairo Hotel Mwanza. |
Leo (jumatano 7/08/2013) timu hiyo toka Rorya itashuka dimba la CCM
Kirumba kumenyana na Chanel Afrika ya Kirumba na kesho alhamisi
kusherehekea nane na zama za sikukuu ya Iddi itachuana na Alliance
Academy Sports Club.