Mamlaka ya Maji safi na maji taka mkoa wa Arusha(Auwsa)imeshindwa kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 100 kutokana na baadhi ya Taasisi za Serikali kushindwa kulipia ankra za maji zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 322
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo mhandisi Ruth Koya wakati akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Maji Binilith Mahenge mapema jana Jijini hapa
Mhandisi Koya alisema kuwa taasisi hizo ni pamoja na Jeshi la Polisi linalodaiwa kiasi cha shilingi Milioni 287 wakati Jeshi la wananchi linadaiwa kiasi cha milioni 7.1 jambo ambalo limechangia kwa kiwango kikubwa sana kufanya mamlaka hiyo kushindwa kufikia malengo yake
Pia alitaja Taasisi nyingine ambazo ni wadaiwa sugu wa mamalaka hiyo ikilinganishwa kuwa ni taasisi za Serikali ni pamoja na Shule ya Arusha(Arusha School)ambayo nayo inadaiwa kiasi cha Milioni 20 huku nayo hospitali ya mkoa nayo ikidaiwa kiasi cha Milioni 26.
“tumejitaidi sana kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu kwa asilimia mia moja lakinim imeshindikana kwa kuwa hizi taasisi za serikali zinatumwamisha hivyo basi tunaomba msisitizo wako Mheshimiwa waziri kwani malengo yetu yakitimia basi wananchi wataweza kupata huduma staili za maji”aliongeza mhandisi huyo.
Katika hatua nyingine mhandisi huyo alidai kuwa mamalaka hiyo imejipanga kukusanya kiasi cha shilingi billion 9.7 kwa kipindi cha mwaka 2013 huku kwa mwezi wakiwa na malengo ya kukusanya zaidi ya shilingi milini 400.
Katika hatua nyingine naibu waziri wa maji Binilith Mahenge alisema kuwa kiwango hicho ambacho kinakusanyawa kwa mwezi ni kidogo hakitoshelezi ikilinganishwa kuwa jiji la arusha ni kubwa hivyo jitihada za kuongeza mapat0 hayo zinahitajika .
Alitaja jitihada hizo kuwa ni npamoja na kuthibiti upotevu wa maji ambao unafanywa na baadhi ya wateja wasio kuwa waaminifu hivyo kusababisha mamlaka hayo kukosa mapato ya uhakika .
Mbali na hayo Naibu waziri huyo aliitaka mamlaka hiyo ihakikishe kuwa inatekeleza mikakati iliyojiwekea ikiwemo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa maji kutoka elfu sitini na tano hadi kufikia lita elfu tisini na tatu ili iweze kuwahudumia wananchi wote wa Jiji la Arusha
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa mamalaka hiyo kuhakikisha kuwa nao wanachangia mapato ya mamlaka hiyo kwa kudhibiti wizi na upotevu wa maji kwani mamlaka hiyo ikiwa na mapato mazuri basi hata maslahi yao nayo yatakuwa vizuri.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia