Ticker

6/recent/ticker-posts

WHY SERENGETI FIESTA NA KILI MUSIC TOUR HAIFANYIKI ARUSHA FUNGUKA MDAU


Ni takribani miaka miwili tokea mashabiki wa burudani mkoani Arusha wakikosa burudani kubwa ya muziki nchini yaniFiesta na kuachwa wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu kutoka kwa wahusika wa burudani hizi.

Fiesta mkoani Arusha imegeuka kuwa hadithi huku mashabiki wa burudani wakizidi kupitwa na matamasha mengi makubwa ya muziki kama Kilimanjaro Music Tour inayozidi kurindima katika baadhi ya mikoa mikubwa hapa nchini.

 Arusha ni moja kati ya maeneo muhimu hapa nchini yanayotoa ma MC wakubwa wanaozidi kunga'ra katika tasnia ya utangazaji na muziki pia.

 Mashabiki walizoea kushuhudia burudani ya Fiesta katika viwanja vya Triple A, Njiro naSheikh Amri Abeid lakini ghafla burudani hii imeingia mitini bila taarifa yoyote kwa mashabiki wao wa jiji la Arusha. Baada ya Fiesta kufanya hivo sasa na Kilimanjaro Music Tour nao wamefuata nyayo hizo hizo.

Niwazi kabisa kuwa kampuni zote hizi za burudani zinamaamuzi sahihi ya kusitisha kufanya burudani zao katika miji kadhaa wanayoiteuwa, lakini kumbukeni kuwa kila sehemu mnamashabiki wenu wanaotamani kuhudhuria burudani zenu kwa wingi kama Arusha.

Kama sii sababu za kimaslahi, basi muwaweke wadau wenu wazi ili msizidi kuwapoteza kabisa katika ulimwengu wa burudani kwani hadi sasa Tanzania tuna matamasha makubwa mawili tuu. Moja Kilimanjaro Music Awards/Kilimanjaro Music Tour na Fiesta.

Sisi kama wadau wa burudani nchini na mkoani Arusha tunapenda kujua ni sababu gani mji wa Arusha haupo katika ratiba ya utoaji wa burudani zenu kama ilivyokuwa imezoeleka na kama inavyofanyika katika miji mingine ya Tanzania?.

Tutafurahi sana kama ujumbe huu utafika katika sehemu hizo husika ili wadau wa burudani Arusha wapate kutuliza nyoyo zao na kuendelea kuunga mkono burudani hizi hapa nchini kama ilivyo mikoa mingine.

Post a Comment

0 Comments