JESHI LA POLIS ARUSHA LAZIDI KUWAKAMATA MAJAMBAZI SUGU

Jeshi  la  Polisi mkoani Arusha limewatia nguvuni watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliohusika katika tukio la tarehe 23 August  majira ya saa nane na nusu mtaa wa Pangani Mjini Kati Arusha,la kuwajeruhi wafanyabiashara wawili wa madini na kupora kiasi cha shilingi Mil.5 na madini yenye thamani ya shilingi Milioni 40.

Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha liberatus Sabas alisema kuwa jeshi la polisi limewakamata watu hao mara baada ya opareshi ya siku mbili iliyofanywa na Jeshi hilo.

Aidha kamanda Sabas aalisema kuwa majambazi hayo yamekamatwa na bastola mbili  aina ya Browing Model  83  CAL .9 no 4738 yenye risasi kumi na bastola ya LAMI yenye risasi 12,gari aina ya Vist yenye namba T368 AUH,Pikipiki aina ya Skygo,namba T352CBW,na Pikipiki nyiongine aina ya Honda  yenye T 464 APH.

Sabas amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Shangai Willium Semboni(38)mkazi wa Sokone one,Alli Habibu Hussein au Dogoo au Sadock(23)mkazi wa Tabata Dar es Saalam,Eugine Donas Mushi maarufu kama Mbuna(28)mkazi wa makao mapya pamoja na Jerome Shirima (29) mkazi wa Sombetini.

Alisema kuwa Wafanyabiashara hao waliojeruhiwa ni pamoja na Aber Musa(35) na Stephen Aloyce(36) wote wakazi wa Sakina jijini Arusha ambao walijeruhiwa na wanaendelea kupatiw matibabu.

Kamanda sabas alisema kuwa  majambazi hao wamekiri kuhusika kwenye matukio mengine ya uhalifu likiwemo kuuwawa kwa mfanyakazi wa kampuni ya Panone ambaye alipigwa risasi.

Kamanda Sabas alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kuendelea kuwafichua wahalifu ambao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya uhalifu jijini hapa.

Jeshi la Polisi bado linaendelea kusaka watuhumiwa wengine wawili ili kuutokomeza kabisa mtandao huo ambapo watuhumiwa hao wametajwa na wenzao ambao wamekamatwa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post