Taarifa zilizo tufikia na kuthibitishwa na Rev. Daniel Kulola ambaye ni mtoto wa Askofu Moses Kulola, Zinasema Askofu Moses Kulola amefariki dunia.
Taarifa hizo zinadai kuwa askofu huyo wa kanisa la EAGT alifariki dunia wakati alipokuwa anapata matibabu katika moja ya hospitali iliopo jijini dar es salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa muda wa wiki moja
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.