Shehe wa mkoa wa Kilimanjaro Alhaj Shaban Rashid akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Moshi Alhaj Ibrahim Msengi kupata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania tawi la Moshi.
Waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania tawi la Moshi kwa ajili ya Waislam katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Wageni mbalimbali wakipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania tawi la Moshi katika viwanja vya Golf vya Moshi club.
Wageni mbalimbali wakipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania tawi la Moshi katika viwanja vya Golf vya Moshi club.
Waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania tawi la Moshi katika viwanja vya Golf vya Moshi club.
Mkuu wa wilaya ya Moshi Dk Ibrahim Msengi akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyofanywa na benki ya Azania tawi la Moshi .
Afisa biashara mwandamizi wa Azania Bank LTD Othman Jibrea akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyofanywa na benki hiyo tawi la Moshi
Shehe wa mkoa wa Kilimanjaro Alhaj Shaban Rashid akiongoza dua baada ya hafla hiyo.
MKUU wa wilaya ya Moshi Dk Ibrahim Msengi amewataka waumini wa dini ya
Kiislam kuendelea kuhubiri amani na upendo katika taifa la Tanzania
hata baada ya kumaliza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Dk Msengi ameyasema hayo wakati wa futari ya pamoja ilioandaliwa na
benki ya Azania tawi la moshi kwa viongozi mbalimbali wa mkoa pamoja
na wateja wake wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha iliyofanyika katika
viwanja vya Golf vya Moshi klabu.
Amesema suala la kudumisha amani na umoja miongoni mwa jamii ni jambo
muhimu na linapaswa kulindwa na kila mmoja kwani amani pekee ndioyo
itachangia kuletea maendeleo kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Naye meneja rasilimali watu na utawala wa Azania Benki ,Bernad Haule
amesema lengo la benki hiyo ni kuimarisha umoja na wateja wao na kuwa
tawi la Moshi limefikia mafanikio waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na
kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumzia hali ya mabenki nchini Haule amesema taasisi za benki
zinapaswa kufanya tafiti na kutoa bidhaa zitakazowavutia wateja
hususan waishio vijijini kwani takwimu zinaonyesha wananchi wengi wa
vijijini hawajajiunga kwenye mfumo wa benki.