Morsi akutana na Catherine Ashton


Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi na mkuu wa EU Catherine Ashton
Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi na mkuu wa EU Catherine Ashton

Wafuasi wa rais aliyetimuliwa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi wameitisha maandamano zaidi  Jumanne huku mwanadiplomasia wa ngazi ya juu katika Jumuiya ya Ulaya akisema kiongozi huyo wa zamani anaishi vizuri japo amezuiliwa.
Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Ulaya Catherine Ashton alisema amezungumza na bw. Morsi kwa njia ya wazi kuhusu mzozo wa kisiasa uliogubika Misri. Bi Ashton alisema mojawapo ya masharti aliyowekea utawala wa muda katika ziara yake ya Misri, ni kuweza kuzungumza na bw. Morsi.

Maafisa nchini humo walimpa nafasi ya kuzungumza na rais huyo wa zamani kwa muda wa saa mbili lakini Ashton hakuweza kubaini ni wapi Mosri anazuiliwa.

 Hii ni mara ya kwanza  kwa mwanadiplomasia wa kimataifa kukutana na kiongozi huyo aliyetimuliwa tangu majeshi ya Misri yalipomkamata na kumweka kizuizini yapata mwezi mmoja uliopita.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia