VITIO VYA MAFUNZO YA KILIMO KUANZISHWA NA ASASI


ASASI ya wakulima wa mazao  ya  maua na mbogamboga nchini  (TAHA) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), linalofadhili Mpango wa Uzalishaji wa Kilimo Tanzania (TAPP), zimekubaliana kuanzisha vituo vya mafunzo ya kilimo cha mazao hayo kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta za umma na binafsi.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini hapa jana,  Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA, Jacqueline Mkindi, alisema mpango huo unatarajiwa kutoa matokeo mazuri kwa wadau wa kilimo cha mazao ya maua na mboga mboga  nchini.
Mkindi alibainisha hivi sasa wapo katika mchakato wa uanzishaji wa vituo hivyo ambapo utahusisha taasisi za serikali za utafiti na mafunzo kama vile Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Taasisi ya Utafiti Uyole mkoani Mbeya, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mazao ya Maua na Mboga mboga  (HORTI-Tengeru), na Kituo cha Utafiti cha Kizimbani Zanzibar katika kuanzisha vituo vya mafunzo ya kivitendo (PTCs).

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia