WANANCHI WA LONGIDO WAPONGEZWA KWA KUJITOLEA KUJENGA JENGO LA POLISI WILAYA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo watatu kushoto akizindua jengo la utawala polisi wilayani longido,jengo hilo lililojengwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapa
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akizindua jengo la utawala polisi wilayani longido,jengo hilo lililojengwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapa
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akizindua jengo la utawala polisi wilayani longido,jengo hilo lililojengwa na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapa
Jengo jipya la utawala Polisi wilaya ya Longido ambalo lilizinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali
Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amewashukuru na
kuwapongeza wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamejitoa na kuhakikisha wanakamilisha
jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido.
Akizindua jengo hilo jana, alisema kwamba litawezesha Jeshi
la Polisi kufanya kazi kwa utulivu sambamba na kukabiliana vyema na masuala ya
uhalifu katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa anajisikia furaha na fahari kuona wadau
wanashirikiana na kuagiza meneja wa Tanesco wilaya ahakikishe ameweka mita ya umeme
ambapo gharama hizo aliahidi atazitoa yeye mwenyewe.
“Lazima tuimarishe mipaka na Polisi wawe na vituo vya uhakika
vya kufanyia kazi ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu na
Jeshi hilo litaendelea kutumia mbinu shirikishi”. Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Bw. Gambo aliwaasa baadhi ya viongozi wa vijiji na
vitongoji pamoja na wananchi kutoficha
wageni ambao wanaishi nchini bila kufuata sheria na kuongeza kuwa yeyote
atakayegundulika anafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.
“Kila kiongozi anapaswa kutambua watu wote wanaoishi katika
eneo lake na kuhakikisha mgeni yoyote amefuata sheria na kama akigundua
(Anaishi bila utaratibu) atoe taarifa kupitia kamati za ulinzi na usalama za
kata ili hatua ziweze kuchukuliwa”. Alisisitiza Bw. Gambo.
Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyeji wa shughuli hiyo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Omari Mkumbo
mbali na kuwashukuru wadau hao, alisema kwamba tukio la uchangiaji na
ukamilishaji wa jengo hilo limeonyesha kwamba wana Longido wana mshikamo wa
hali juu.
Kamanda Mkumbo alisema kwamba wananchi waendeleze mshikamo
huo ili kuweza kuimarisha kituo kingine cha Polisi kilichopo tarafa ya Kamwanga
na kutaja majengo mengine ambayo yanajengwa na kukaribia kukamilika kwa hamasa
ya Mkuu wa mkoa kuwa ni kituo cha Polisi cha Kwa Morombo pamoja na kituo cha
Polisi cha Utalii ambacho ujenzi wake unafadhiliwa na TATO (Tanzania Tourist
Operators).
“Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha uhalifu
unakomeshwa na japokuwa takwimu za matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo yapo
chini lakini bado kuna tatizo la madawa ya kulevya aina ya Bhangi na Mirungi
hivyo wananchi endeleeni kutoa ushirikiano kwa askari kwani madhara ya madawa
hayo ni makubwa”. Alisema Kamanda Mkumbo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Daniel Chongolo
alisema ongezeko la ukamataji wa madawa ya kulevya umetokana na udhibiti mzuri
na kuahidi kuimarisha zaidi usalama kwa kutumia Polisi na vyombo vingine vya
usalama huku akitoa shukrani zake kwa Kamanda wa Polisi mkoa kwa kutoa gari
ambalo litasaidia kuimarisha ulinzi katika tarafa ya Kamwanga.
Awali akitoa taarifa ya uhalifu pamoja na mchakato wa ujenzi
huo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joswam
Israel Kaijanante alisema kwamba ujenzi huo umegharimu zaidi ya Milioni 80 ambazo
zilichangwa na viongozi, askari pamoja na wananchi na kuongeza kwamba bado
jengo hilo halina samani na “Kompyuta , Printer” pamoja na mfumo wa maji taka
ambapo gharama zake ni Milioni 16.
Mchakato wa ujenzi wa jengo hilo ambao una ofisi tatu ambazo
ni za Mkuu wa Polisi wilaya, Mkuu wa Upelelezi wilaya na Mwendesha Mashtaka wa
Polisi ulianza mwaka 2015 na kukamilika mwezi Julai mwaka huu uliwashirikisha
kikamilifu jumla ya wadau wapatao 20 ambao pia walipewa vyeti vya shukrani.
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia