MATUKIO MBALIMBALI YAKIONYESHA MAVETERANI WALIOPIGANA VITA VYA KAGERA WALIVYO ATHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA KWA KUWEKA SILAHA ZA JADI KWENYE BUSTANI YA MNARA WA MASHUJAA ILIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA

 


 Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka  vijana  wa Tanzania kuwa wazalendo  pamoja  kuifia nchi yao Ili kuendelea kulinda na kuenzi amani ya nchi yetu

  Aliyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa na baadhi ya wananchi katika sherehe za  maadhimisho ya  siku ya mashujaa ambapo kwa Mkoani wa  Arusha imefanyika katika bustani ya mashujaa iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha



Alisema kuwa  kumbukumbu ya mashujaa walioipigania nchi ni fundisho kwa watanzania  kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano ili nchi yetu iwezo kusonga mbele.

Alibainisha kuwa mashujaa hao waliweza kuipigania nchi ndio maana hadi  leo nchi yetu ina amani na utulivu mwingi.










Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akibadilishana mawazo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana mara baada ya zoezi la uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime katika sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa yaliyofanyika leo ambapo kwa mkoa wa Arusha yamefanyikia katika bustani ya Mnara wa Mashujaa iliopo ndani ya halmashauri ya Jijini Arusha na kuuthuriwa na baadhi ya Mavetenari waliopigana Vita vya Kagera



About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia