Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA).
Yamesemwa hayo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella alipokuwa akizungumza na wataalamu na wadau wa michezo kwa Mkoa wa Arusha.
Amesema ugeni huo ni mkubwa sana katika Mkoa wetu kwani wageni takribani 3,153 wanatarijiwa kuhudhuria.
Kama Mkoa umeshajipanga kupokea ugeni huo huku mazingira ya maradhi na usalama yapo vizuri.
Amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuwa wakarimu kwa wageni hao kwani ni njia ya kukuza Utalii.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Musa amesema michezo hiyo itapanua zaidi wigo wa Utalii katika Mkoa kwani kuna wageni kutoka nchi takribani 6 za Afrika Mashariki huku nchi ya Malawi ikiwa kama mgeni mwalikwa.
Mratibu wa FEASSSA bwana George Mbijima amesema mashindano hayo yataanza Septemba 14 hadi Septemba 23 na yatafunguliwa rasmi Septemba 18.
Amesema jumla ya wanamichezo 2453 , walimu na viongozi 700 wanatarajia kushiriki katika michezo hiyo.