MKE WA HAYATI MREMA HAAIDI KUWALEA WATOTO WOTE WA MUME WAKE ,HADI SASA KESHAPOKEA WATATU




Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP Hayati Augustino Lyatonga Mrema, Doreen Mrema amesema kuwa hadi sasa ameshapokea watoto wa Hayati Mrema zaidi ya watatu (3) ambao walikuwa hawajatambulika kwenye Familia na ameahidi ataendelea kuwapokea na kuwalea kama mama yao na yupo Tayari kuendelea kuwapokea endapo tu ni kweli watakuwa ni watoto wa Mzee Mrema


Doreen amesema hayo jana wakati akizungumza na vyombo vya habari Mjini Moshi ambapo pia ametoa shukrani zake kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na watu binafsi kwa kuwa nao kipindi chote cha msiba.


"Alinieleza Nisiogope na niwapokee na niombe radhi kwenu, niwakumbatie na niwalee kama mama yao kama ambavyo yeye angewalea na ninamshukuru Mungu nimeendela kuwapokea watoto ambao walikuwa bado hawajambulika kwenye familia na sasa nimeshapokea zaidi ya watoto watatu (3). Mimi kama mama nitaendelea kuwapokea na kuwakumbatia kama ambavyo Mume wangu Mpenzi alivyoniasa siku 2 kabla ya kifo chake" - Mjane wa Mrema, Bi. Doreen Mrema 


Aidha amewahakikisa Watanzania kuwa ataendelea kumuenzi mume wake mpenzi (Hayati Mrema) na kuishi vile alivyomuasa na muda sahihi wakizungumza ukifika ataeleza ukweli juu ya maneno yanayoongelewa katika mitandao ya kijamii.


"Muda sahihi ukifika nitasema ukweli wote,yapo maneno mengi yanayo ongelewa na watu na mengine yameandikwa kwenye vyombo vya habari na mtandaoni,ila muda ukifika nitasema,siogopi na Mzee Mrema alisema nisiogope hata wakati hayupo"Doreen Mrema

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia