SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAKAMPUNI YANAYOTUMIA KIGEZO CHA FURSA KUWAKANDAMIZA VIJANA
Wilaya ya Arumeru imepiga marufuku makampuni na watu binafsi wanaotumia kigezo cha fursa kuwatapeli na kuwakandamiza vijana kuacha mara moja
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Vijana duniani yaliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, mwakilishi wa Mkuu wa ya Arumeru Mwl.Marcus Nazi ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi wa halmashauri hiyo ametoa wito kwa vijana kuitumia vema fursa mbalimbali kujikwamua kiuchumi ikiwemo fursa ya mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri .
Mwl.Nazi alisema serikali imeweka mikakati kupitia sera mbalimbali za kuwaletea vijana maendeleo kwa kuzingatia kundi la vijana ni kundi kubwa kwani tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 65% ya waishio bara ni vijana ambapo ametoa wito kwa wadau kuungana na serikali kuwasaidia vijana na si kuwakwamisha kwani Serikali wilayani humo haitosita kuwachukulia hatua makampuni au watu binafsi wanaowakandamiza vijana kwa kigezo cha fursa .
Elisante Nnko ambaye ni miongoni mwa vijana walioshiriki maadhimisho hayo ametoa wito kwa vijana kufuata imani waliojengewa kwenye jamii na serikali kwa kuchapa kazi kwa weledi na bidii.
Maadhimisho hayo ya siku ya vijana yaliyofanyika katika viwanja vya MS TCDC yamewezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushirikiana na wadau wa Mashirika ya SOS CHILIDREN'S VILLAGES, VOICE OF YOUTH TANZANIA, DUSAFO, SAVE AFRICA TANZANIA ,TAMIHA,KAMBELE
Ikumbukwe kila mwezi Agosti Dunia huadhimisha siku ya Vijana,ikiwa lengo ni kukumbuka mchango wa vijana katika kukuza maendeleo huku kaulimbiu ya mwaka ikisema "Kuelekea 2030: Tanzania ya viwanda,boresha elimu Kwa vijana,kwa maendeleo ya Taifa".
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia