VIONGOZI WA DINI MILA WATAKIWA KUHAMASISHA JAMII KUSHIRIKI ZOEZI LA SENSA


 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango ametoa  wito kwa viongozi wa dini, viongozi wa mila, wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ,Waheshimiwa Madiwani na Watendaji wa Serikali  kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la sensa ili Kupata takwimu  za msingi zitakazosaidia kuainisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee ili kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti  na viongozi  wa Tarafa ya Poli na King'ori Ruyango alisema   Agosti 23/ 2022 kila Mtanzania aliyelala ndani ya Wilaya hiyo awe Mkazi au la  anapaswa kuhesabiwa  ambapo amehimiza viongozi kuwahamasisha na kuwaelimisha  wananchi kutoa ushirikiano kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi 


 " nitoe wito kwenu viongozi mkawe  wazalendo  kwani Tanzania inajengwa na watanzania hivyo tushirikiane kuhakikisha zoezi la sensa linafanikiwa katika maeneo yetu" amehimiza Ruyango.

Nae Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Meru Daudi Wengi  akimwakilisha mratibu wa Sensa alisema  kuwa  tarehe 23 Agosti 2022 itabaki kuwa tarehe rejea ya Sensa ambapo watu wote waliyolala usiku wa kuamkia tarehe 23 watahesabiwa ambapo amewataka   wakuu wa  kaya kuwa na taarifa zote muhimu za watu waliolala kwenye kaya yake usiku wa kuamkia tarehe ya sensa ambapo amebainisha taarifa hizo ni umri, jinsi,hali ya ndoa,elimu ,shughuli za kiuchumi ,umiliki wa vitambulisho vya taifa  .

Kwa upande wao viongozi wa dini na Mila waliohudhuria  mkutano wa uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi wametoa wito kwa jamii kushiriki zoezi la Sensa ili kutoa taarifa sahihi ili kuwezesha Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi kulingana na idadi ya watu ya eneo husika


" nitoe wito kwa wananchi  kushiriki kuhesabiwa katika zoezi la sensa pia sisi kama viongozi wa mila  hatutaruhusu mtu yeyote kuleta Mgogoro kwenye zoezi la Sensa" amesema Hezron Sumary  Mshili Mkuu Meru

Naye Ramadhan Omary Sheik Wa Usa-River na Amani Halisi Kuhani  alisema kuwa wao kama viongozi wa dini watahakikisha jamii inaendelea kuhamasika na kushiriki katika zoezi la Sensa kwa maendeleo ya nchi.

Kwa upande wao viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji pamoja na viongozi wengine wa halmashauri hiyo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki  wametoa wito kwa wananchi kujitokeza kuhesabiwa kwa kutoa taarifa sahihi zitakazotumika kuwaletea maendeleo

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia