TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA YAMTANGAZA RUTO KUWA RAIS MTEULE WA NCHI HIYO
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza Makamu wa rais William Ruto kuwa Rais mteule.
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imemtangaza makamu wa rais William Ruto kuwa rais mteule, kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, akimshinda mwanasiasa wa muda mrefu na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Hata hivyo zoezi hilo limekumbwa na sintofahamu baada ya makamishna wanne wa tume ya IEBC kutangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi wa rais wakidai kuwa mchakato huo umekosa uwazi katika hatua za mwisho.
Ruto amepata asilimia 50.49% dhidi ya asilimia 48.8 ya Odinga.

0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia