BLUE SKY NA UPENDO WAHITIMISHA DARASA LA SABA, WASISITIZA ELIMU NA MAADILI


Afisa Masoko wa shule  ya Blue  sky pamoja upendo Erastus Majogoro akiongea na waandishi wa habari  juu ya huduma wanazotoa shuleni apo

Na Woinde Shizza, Arusha

Shule ya Mchepuo wa Kiingereza Blue Sky   na shule ya Upendo ambazo ni taasisi shirika, zimefanya mahafali ya pamoja ya darasa la saba ambapo Blue Sky imehitimisha mahafali ya tisa na Upendo mahafali ya tano.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na wazazi, walezi na wageni waalikwa, jumla ya wanafunzi 26 wa darasa la saba kutoka shule ya Upendo walihitimu rasmi na kukabidhiwa vyeti vya pongezi kwa kutimiza hatua muhimu ya safari yao ya kielimu.
Mkuu wa Shule ya Upendo Elias Ally  akiongea na waandishi wa habari 

Mkuu wa Shule ya Upendo   Elias Ally alisema shule hizo mbili zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma ambapo katika mtihani wa kitaifa wa mwaka 2024 walipata wastani wa Daraja A. Alisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na kuzingatia ufundishaji wa masomo ya kawaida pamoja na malezi ya kidini na maadili mema.

Mkuu wa Shule ya Blue Sky, Julius Michael,  akiongea na waandishi wa habari 

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Blue Sky, Julius Michael, alisema shule hiyo inajulikana kwa kutoa huduma za bweni na kutwa, huku ikiwapokea wanafunzi kutoka makundi mbalimbali wakiwemo yatima, watoto kutoka familia zisizojiweza na pia wanafunzi wanaosomeshwa na wazazi wao au wafadhili.

“Shule yetu ilianzishwa ili kumsaidia mzazi wa kipato cha chini aweze kupata nafasi ya kumpeleka mtoto wake katika mazingira bora ya kusomea na kujifunza maadili,tunawaandaa watoto kuwa watu wenye mchango chanya katika jamii baada ya kumaliza masomo yao,” alisema Michael.

Aliongeza kuwa ni wajibu wa wazazi kushirikiana na shule katika kuhakikisha watoto wanalelewa kwenye misingi ya maadili, hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto nyingi za kimaadili na kitabia.

Naye Afisa Masoko wa shule hizo Erastus Majogoro alihimiza wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye shule hizo akibainisha kuwa ada zao ni nafuu na zinaweza kulipwa kwa awamu hadi sita 

 Alisisitiza kuwa shule hizo hutoa elimu bora darasani, malezi ya kidini na mafunzo ya jinsi ya kuishi kwa usawa katika jamii. 

Naye mmoja wawanafunzi  waliehitimu  Patrick Samwel alisema kuwa elimu  na miongozo aliyoipata ataitumia vyema ,na atafuata maadili yote na mafunzo aliofundishwa kipindi akiwa shuleni apo ,huku akiwasisitiza wenzake kuendelea kusoma kwa ajili ya Maisha yao ya baadae.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia