JUMA RAIBU ATEULIWA KUWANIA UDIWANI KATA YA BOMAMBUZI



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua tena Juma Raibu kugombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi, katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.


Uteuzi huo unakuwa ni mara ya tatu kwa Raibu kuteuliwa na chama chake kuwania nafasi hiyo, jambo linalotafsiriwa kama ishara ya kuendelea kuaminiwa na CCM pamoja na wananchi wa Moshi Mjini.



Akizungumza baada ya uteuzi huo, Raibu alisema anashukuru kwa heshima aliyopewa na chama chake na kuahidi kuendelea kushirikiana na wananchi wa Bomambuzi kusukuma mbele maendeleo ya kata hiyo.


Alisisitiza kuwa kipaumbele chake ni kuimarisha huduma za kijamii, kuendeleza miundombinu, na kuhakikisha wananchi wanapata elimu bora na fursa za kiuchumi.


Baadhi ya wananchi waliozungumza walisema uteuzi huo unaonesha mshikamano wa chama na wananchi, huku wakieleza kuwa Raibu amekuwa kiongozi aliye karibu nao na mara zote husikiliza changamoto zao.


Uteuzi huu unatajwa kuongeza hamasa ndani ya CCM kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa, ambapo chama hicho kimepanga kushinda kata zote za

 Moshi Mjini.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia