Vijana wakiwa na mabango kupinga uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji. |
Upandaji miti kwaajili ya utunzaji wa mazingira |
Ubomoaji wa nyumba ukiendelea |
Wananchi wakikagua chanzo kilichogeuzwa shamba |
Arumeru.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki,wilayani
Arumeru,wamebomoa nyumba moja iliyojengwa kwenye chanzo cha maji ili
kunusuru vyanzo hivyo ambavyo viko hatarini kukauka kutokana na ujenzi
usiozingatia utunzaji wa mazingira.
Wananchi
waliotekeleza hatua hiyo,Steven John na Frank Nnko walisema kuwa
wamechukua uamuzi huo baada ya serikali kushindwa kuwachukulia hatua za
kisheria watuhumiwa wa uvamizi wa vyanzo vya maji .
Nnko
alisema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu kutokana na kuwa wananchi
ndio waathirika wakubwa wa kukauka kwa vyanzo vya maji na kwamba
wameamua kujichukulia sheria mkononi na hawatasita kufanya hivyo kwa
wananchi wengine watakaokiuka utunzaji wa mazingira.
Alifafanua
kuwa kitongoji cha Momela ndicho chanzo kikuu cha maji katika Kata za
King'ori,Makiba na Ngarenanyuki hivyo kuendelea kuwaachia wananchi
wachache kuharibu mazingira kunaweza kugeuza eneo lote jangwa jambo
ambalo linaweza kuhatarisha uhai wa watu na viumbe hai.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Maji bonde dogo la Ngarenanyuki ,Aminieli Mungure alisema kuwa vyanzo
hivyo vimekua vikiharibiwa kwa kukosa usimamizi hivyo wakati umefika
wa jamii kuamka na kuvilinda kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aliongeza
kuwa Bonde dogo la Ngarenanyuki linahudumia vijiji vinne ambavyo ni
Ngabobo, Olkung’wado,Uvizo na Ngarenanyuki na kuwa wataanza kuwaelimisha
wananchi umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.