WAMILIKI WA MAKAMPUNI YA UTALII WATAKIWA KUWAPA KIPAUMBELE WATANZANIA

Wamiliki wa makampuni ya utalii nchini wametakiwa kuwapa kipaumbele watanzania kwa kutumia magari yao ili kuwabeba na kuwawezesha nao watembelee hifadhi za Taifa kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani.
Wito huo umetolewa juzi na mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Beatrice Kessy, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na suala la watalii wa ndani kupatiwa usafiri ili kutembelea mbuga za wanyama.
Akizungumza katika hifadhi hiyo ya Tarangire iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara, Kessy alisema makampuni ya utalii yanatakiwa kuwageukia watalii wa ndani kipindi ambacho siyo cha msimu wa watalii wa kigeni kuwepo kwa wingi.
Alisema japokuwa gharama za kuingia kwenye hifadhi za Taifa siyo kubwa kwa watanzania, wengi wao wanashindwa kuzitembelea na kufanya utalii wa ndani kutokana na kutokuwa na usafiri wa kuwafikisha na kuwatembeza hifadhini.
“Waanzishe huo utaratibu na wengi watachangamkia hiyo fursa, mbona Loliondo kwa babu walikuwa wanatoa magari yao kwa sh700,000 hapa watachanga sh50,000 kwa watu nane sh400,000 siyo mbaya,” alisema Kessy.
Hata hivyo, alisema tangu mwaka 1993 hadi mwaka huu, watalii wa ndani 519,673 walitembelea hifadhi ya Taifa ya Tarangire tofauti na watalii wa nje 1,140,016 na jumla ya watalii waliotembelea hifadhi hiyo kuwa 1,659,688.  
 “Bado tuna changamoto kwa watalii wa ndani kutotembelea kwa wingi hifadhi kutokana na kutokuwa na usafiri, hivyo makampuni ya utalii wawape kipaumbele watalii wa ndani kwa kuwapunguzia bei,” alisema Kessy.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia