AKAGUA MIRADIILIOTOKELEZWA KUTOKANA NA ILANI YA UCHAGUZI

Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndengasso Ndekubali ametembelea miradi mbalimbali ya Kata ya Mirerani, Wilayani Simanjiro na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama hicho kwa mwaka 2010 hadi 2015.

Ndekubali alitembelea kata hiyo na kukagua ujenzi wa madarasa matatu ya shule mpya ya sekondari Songambele, ambayo inatarajia kuanza kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2014.

Pia, alikagua ujenzi wa vyoo, madarasa, ofisi ya walimu wa shule ya Tanzanite na kuelezwa kuwa Diwani wa kata hiyo Justin Nyari alichangia fedha zake sh1.5 milioni kwa ajili ya ujenzi wa choo na kisima cha shule ya msingi Songambele.

“Kwa nafasi ya pekee nakupongeza Diwani wa kata ya Mirerani Nyari, kwa kutoa fedha zako binafsi kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii, ikiwemo kujenga wa madarasa mawili ya shule ya msingi Tanzanite,” alisema Ndekubali.

Katibu huyo, pia alikagua na kuridhika na ujenzi wa barabara za mji mdogo wa Mirerani zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha changarawe, kwa gharama za halmashauri ya wilaya ya Simanjiro.

Hata hivyo, Ndekubali aliuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo, kukarabati madarasa matatu ambayo yameweka ufa na kutishia uhai wa wanafunzi katika shule ya msingi Songambele.

“Huku ni kuchezea fedha za Serikali yaani madarasa yajengwe juzi mwaka 2008 leo yabomoke na kusababisha wanafunzi kuacha kusoma kwenye hayo madarasa na kupeana zamu za kuingia darasani,” alisema Ndekulali.


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia