AKAGUA MIRADIILIOTOKELEZWA KUTOKANA NA ILANI YA UCHAGUZI
Katibu wa CCM Mkoa wa
Manyara, Ndengasso Ndekubali ametembelea miradi mbalimbali ya Kata ya Mirerani,
Wilayani Simanjiro na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama hicho
kwa mwaka 2010 hadi 2015.
Ndekubali alitembelea kata
hiyo na kukagua ujenzi wa madarasa matatu ya shule mpya ya sekondari Songambele,
ambayo inatarajia kuanza kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza kwa
mwaka 2014.
Pia, alikagua ujenzi wa
vyoo, madarasa, ofisi ya walimu wa shule ya Tanzanite na kuelezwa kuwa Diwani
wa kata hiyo Justin Nyari alichangia fedha zake sh1.5 milioni kwa ajili ya
ujenzi wa choo na kisima cha shule ya msingi Songambele.
“Kwa nafasi ya pekee
nakupongeza Diwani wa kata ya Mirerani Nyari, kwa kutoa fedha zako binafsi kwa
ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii, ikiwemo kujenga wa madarasa mawili ya
shule ya msingi Tanzanite,” alisema Ndekubali.
Katibu huyo, pia alikagua
na kuridhika na ujenzi wa barabara za mji mdogo wa Mirerani zinazoendelea
kujengwa kwa kiwango cha changarawe, kwa gharama za halmashauri ya wilaya ya
Simanjiro.
Hata hivyo, Ndekubali
aliuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo, kukarabati madarasa matatu
ambayo yameweka ufa na kutishia uhai wa wanafunzi katika shule ya msingi
Songambele.
“Huku ni kuchezea fedha za
Serikali yaani madarasa yajengwe juzi mwaka 2008 leo yabomoke na kusababisha
wanafunzi kuacha kusoma kwenye hayo madarasa na kupeana zamu za kuingia
darasani,” alisema Ndekulali.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia