WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA DR. WILLIAM MGIMWA AZINDUA NEMBO NA TOVUTI YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF, JIJINI ARUSHA


 Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo Mpya ya PPF iliyoambatana na Tovuti Mpya ya PPF.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa PPF,Dk. Aggrey Mlimuka na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio.
 Hivi ndivyo inavyoonekana Nembo Mpya ya PPF. 
 Nembo na Tovuti.
  Kushoto ni Mhe. Godbless Lema na Mhe. Joshua Nassari wakifuatilia kwa umakini Hotuba ya Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 23 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Waziri wa Fedha,Dkt William Mgimwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua.
Bw. Bonda Nkinga akitoa Ushuhuda wake wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kuwasaidia watoto zake kusoma kupitia Fao la elimu.
Kijana Peter William Mulokozi ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Mzumbe akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Baba yake kupoteza maisha ghafla.PPF ambao ni Mfuko pekee unaotoa fao la Elimu nchini endapo Mwanachama anakuwa amefariki akiwa kwenye ajira.PPF imeweza kumsaidia kijana huyu kusoma mpaka hapo alipofikia.
Kijana Pascalia Nsatto ambaye ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Kimataifa ya Moshi akitoa ushuhuda wake mbele ya Wanachana na Wadau wa PPF waliohudhuria kwenye Mkutano wa 23 wa Mwaka,juu ya PPF ilivyoweza kumsaidia yeye kusoma,mara baada ya Wazazi wake wote wawili kupoteza maisha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post