Kesi ya Uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mbunge Lema imefutwa!
Upande wa mashitaka, Jamhuri imeiomba Mahakama kufuta kesi ya
uchochezi iliyokuwa ikimkabili Mhe. Lema. Hii ni ile kesi ya kudaiwa
kuchochea vurugu Chuo cha Uhasibu Arusha.
"Nimeshinda
kesi tena! Kwa kweli Mungu anatupenda sana na tutaendelea kupambana
kutafuta haki bila hofu. Miili yetu na nafsi zetu zimepoteza maumivu kwa
sababu ya mateso yaliyojaa uongi na hila. Hata hivyo tutaendelea na
kelele za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo
yetu kuu" alisema Mbunge Lema , katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha mara baada
ya kushinda kesi dhidi yake na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa
Mulongo zikihusisha kilichodaiwa kuwa uchochezi kwa wanafunzi wa Uhasibu
Arusha wamzomee Mulongo na kufanya fujo... Kesi hiyo imefutiliwa mbali
baada ya washitaki kuomba hivyo pamoja na kwamba leo ndio ilikuwa siku
ya kuanza kusikiliza ushahidi wa Mkuu wa Mkoa, Dean of Students, Makamu
Mkuu wa Chuo na Maofisa wa Polisi wakiongozwa na OCD Muroto.
|