Washindi wa shindano la
Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling (kushoto) na Mwenzake Mark wakitembezwa
na kuangalia namna walemavu wa kituo cha Shanga River House cha jijini Arusha,
washindi hao waliopatikana kupitia kampuni ya My Destination walikuwa nchini na
kutembelea vivituo mbalimbali vya utalii na kukagua miradi mbalimbali kama
hiyo.
Mshindi wa shindano la
Biggest Baddiest Bascket, Allex Ayling akipuliza kioo kilicho yeyushwa tayari
kwa kutengenezwa chombo chochote ambavyo hutokana na taka ngumu zinazozalishwa
na binadamu ikiwa ni moja ya shughuli zinazo fanywa na walemavu katika kituo cha
shanga river house cha jijini Arusha.
Allex na Mark wakipewa maelezo ya shughuli za
kituo.
WADAU mbalimbali wa utalii
wa ndani na nje ya nchi wametakiwa kuutangaza utalii wa Tanzania katika maeneo
yao ili kuwavutia watalii wengine kuzidi kufika kwa wingi hapa nchini kujionea
maliasili zilizopo na kuchangia pato la taifa kwa ujumla.
Hayo yalielezwa jana na
Afisa Mtendaji wa TATO ,Sirili Akko wakati akizungumza na wadau wa maswala ya
utalii waliohudhuria katika hafla ya kuwapongeza vijana wawili walioshinda
shindano lililoandaliwa na kampuni ya My Destination lililoshirikisha washiriki
122 ulimwenguni.
Aidha alisema kuwa
,Tanzania ni nchi ambayo imebahatika kupata vivutio mbalimbali vya utalii hivyo
kuwavutia watalii kufika na kujionea maliasili zetu, hivyo hawana budi
kuutangaza utalii wetu katika nchi zao ili kuendelea kukuza utalii zaidi kwa
nchi za Afrika.
Alisema kuwa, shindano hilo
lilihusu mshiriki kuchagua vitu ambavyo wangependa kufanya maishani kabla
hawajafa ndipo vijana hao wawili waliposhiriki katika shindano hilo na kuoanisha
kuwa wao wangependa kutembea dunia nzima na kujionea maajabu yaliyopo katika
vituo mbalimbali.
‘baada ya vijana hao
kushiriki shindano hilo walishinda na kupewa nafasi ya kuchagua kutembelea nchi
25 kati ya 80 ambazo katika hizo nchi 25 walichagua nchi tatu za Afrika ikiwemo
kutembelea Tanzania,Zimbabwe,na Afrika ya kusini na ndo maana wapo hapa leo
tayari kwa kuanza zoezi hilo’alisema Akko.
Aliongeza kuwa, kitendo cha
wao kuchagua Tanzania kati ya nchi 25 kimewafariji sana wao kama wadau wa
utalii kwani imeonyesha jinsi ambavyo utalii wa nchi yetu unaweza kutangazwa na
watalii mbalimbali na hatimaye kuweza kupata wageni wengi zaidi kwa kujionea
maliasili zilizopo katika maeneo yetu.
Nao vijana hao walioshinda
shindano hilo kutoka Calfonia Alex Ayling na Mark Ayling walisema kuwa,
shindano hilo waliweza kushinda baada ya kukithi viwango vya shindano hilo na
hatimaye wamefurahia sana kushinda kwani mchuano uliwashirikisha watu mbalimbali
ulimwenguni.
Alex alisema kuwa, lengo la
kuchagua Tanzania miongoni mwa nchi tatu za Afrika ambazo wangependa kutembelea
ni kutokana na uoto wa asili uliopo katika maeneo mbalimbali ikiwemo hifadhi ya
Serengeti kwa ajili ya kujionea wanyama mbalimbali kama sehemu ya uchaguzi wao
.
Alisema kuwa,katika maeneo
hayo yote watakayotembelea watakuwa wakichukua mikanda mbalimbali kwa ajili ya
kuirusha kwenye mtandao na hatimaye watu mbalimbali kuweza kujionea vivutio
mbalimbali vilivyopo katika vituo watakavyotembelea.
Mark alisema kuwa, wamekuwa
wakifuatilia vitu mbalimbali vinavyoendelea Tanzania ikiwemo wanyama mbalimbali
wa kuvutia , pamoja na kufuatilia makabila ya wamasai ambayo watakuwa na nafasi
ya kuwatembelea na kuweza kujifunza maswala mbalimbali kutoka
kwao.
walipewa zawadi na marafiki
mbalimbali.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia