Katika mazungumzo hayo Diamond alitaja mambo haya makuu matano yaliyosababisha mpaka aamue kurudisha vikosi kwa mwanadada Sepetu.
Sababu ya kwanza (1) – UKARIMU WA WEMA
Diamond alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.
“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.
Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.
“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.” Alisisitiza Diamond.
Sababu ya Pili (2) – Pamoja na Ukarimu – Mapokezi ya nguvu aliyopewa
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘Za Hatari’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.
Sababu ya tatu (3) – Ujasiri wa wema kwenda Hong Kong na kujiandaa kuwa mwenyeji wake.
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’
Sababu ya nne (4) – Mapenzi mazito aliyopewa huko Uchinani na Wema
Diamond alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye.
Sababu ya tano (5) - Bado alikuwa na mawazo ya kupata mtoto na Wema
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.
Penny Je, hatima yake nini?
Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.