Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ya
habari mkoani Kilimanjaro.
SIKU moja
baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas
Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi ,mkuu
huyo amejitokeza mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma
hizo.
Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake
aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa
yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha sh Mil 500
zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa
Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi kilipojengwa
kiwanda cha kutengeneza Saruji.
Alisema tuhuma
zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na
kwamba ni za kisiasa huku akitaja
sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe
haramu katika wilaya ya Rombo
pamoja na Urejeshwaji wa wafanyabiashara katika soko la kati
la mjini Moshi.
“Nataka niwaambie hii ni siasa,zipo issue nyingi
zilizochangia kuibuka kwa haya
mambo ,lakini nawaambieni mbili tu,Issue ya kwanza
Pombe Rombo,na msimamo wangu juu ya
Pombe Rombo ndio imeza hii,la pili ni soko la Moshi
mjini,watu wana agenda zao kwenye soko hilo
,wananchi wamerudi pale
,imewaumiza watu.”alisema Gama.
“Watu walitaka
Pombe ya Gongo iharalishwe,mimi nimesema hadharani anayetaka pombe ya Gongo ihararishwe si mwenzetu
mu mshughulikie kwa maana si mwenzetu
sasa hili limeleta nongwa”aliongeza Gama.
Akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma hizo ,Gama amekiri
mtoto wake aliyetajwa kwa
jina la Mayunga Leonidas Gama kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda hicho huku akihakikisha
kiwanda hicho kinajengwa katika mkoa
wa Kilimanjaro badala ya Bagamoyo kama walivyo pendelea wawekezaji
hao.
“Kiwanda cha saruji kinachojengwa pale Rombo,
nilikuwa na uwezo wa kukipeleka popote
ninapotaka mimi, lakini mimi binafsi ndiye niliyefanya juhudi kiwanda kile kijengwe
Kilimanjaro, mimi binafsi na wala sio mtu mwengine, nimefanya juhudi hizo kwa
lengo la kuongeza ajira kwa wananchi na kuinua uchumi wa mkoa huu”,
alisema Gama .
“Historia ya Kiwanda hiki iko wazi, na
nililipeleka hadi kwenye kikao cha ushauri wa mkoa (RCC),nanaomba nieleweke
kwamba, ni juhudi zangu na za mtoto
wangu, nilitamka kwenye kikao kile na wala
sikuficha, mtoto wangu ambaye
ametajwa yeye ana rafiki yake wa kichina, wala si kweli kwamba hii
kampuni mimi nimekwenda kuichukua China kwa gharama za serikali” aliongeza Gama.
Alisema katika kikao hicho (RCC), Mbunge wa Rombo,
Joseph Selasini, Mbunge wa Vunjo,
Dkt. Augustino Mrema na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, walishiriki katika kikao
hicho na kwamba baada ya mvutano
ndipo makubaliano yakawa kiwanda kijengwe wilaya ya Rombo .
“Toka siku ile mimi kama mkuu wa mkoa nikakabidhi
madaraka wilaya yaRombo,kwa hiyo
shughuli zote za ujenzi ,shughli zote za kutafuta viwanja ziifanywa na halmashauri ya wilaya ya
Rombo na sio Gama”alisema
Gama.
Alisema waliolipa fidia na kununua viwanja ni
halmashauri ya wilaya na hata eneo |
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia