DAVIS MOSHA ATANGAZA KUTOGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI.
| Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo. |
| Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio. |
| Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge . |
| Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo. |
| Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia. |
| Wengine walitishia kujinyonga mbele yake. |
| Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge. |
| Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea. |
| Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio. |
0 Comments:
إرسال تعليق
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia