SALAMU ZA POLE TOKA CHADEMA ARUSHA KUHUSINA NA KIFO CHA MGOMBEA UBUNGE WA ACT-WAZALENDO ARUSHA MJINI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHADEMA-LOGOChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kimesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa
wakongwe nchini, Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye alipata kuwa Mwanachama na Diwani Kata ya Kimandolu kupitia CHADEMA katika Wilaya hii.
Tumepokea kwa masikitiko makubwa na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Estomih Jonas Mallah ambaye tumejulishwa kuwa aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa, Oktoba 9, 2015, katika Hospitali ya Rufaa- KCMC, Mkoani Kilimanjaro. Ni dhahiri Wanademokrasia tumeondokewa na mtu muhimu katika kipindi
muhimu.
Tunatuma salamu za dhati kuomboleza kifo cha Ndugu yetu Estomihi Jonas Mallah kwa familia, Viongozi na Wanachama wa chama cha ACT- Wazalendo.
Kwa pamoja tunamwomba Mungu mwenyeenzi, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya Marehemu Estomih Jonas Mallah. Amen
Lewis Emmanuel Kopwe
Kaimu Mwenyekiti
Wilaya ya Arusha Mjini
10/09/2015









About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

إرسال تعليق

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia