Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF.
Washirika wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
Washirika hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).
Wakitoa taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.
Walisema kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.
“Kuna mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.
“Tunaangalia changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,
“Mpango huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema Rodriguez.
Kiongozi wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
Wanufaikaji wa mpango wa PSSN wakisoma risala kwa wageni.
Mmoja wa wanufaikaji wa mpango wa PSSN akitoa maoni wakati wa mkutano na washirika wa maendeleo waliotembelea kijiji chao.
Mwenyekiti kijiji cha Vikuge, Vitus Mchami akitoa salamu kwa niaba ya wanakijiji kwa ugeni huo.
Baadhi ya wanakijiji cha Vikuge wanaonufaika na mradi wa PSSN waliohudhuria mkutano huo.
Zoe Glorious (kulia) kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akifanya mahojiano na Mnufaikaji wa kijiji cha Vikuge, Bi. Halima ambaye aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kuanzisha biashara ya kufuga bata ambayo imemuwezesha kuendesha maisha yake na kumuingizia kipato.
Bi Halima akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wake wakati wa ziara ya washirika wa maendeleo nchini walipomtembelea nyumbani kwake.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland nchini, Milma Kettunen (kulia) akinunua moja ya bidhaa iliyotengenezwa na ukili kutoka kwa wakinamama wa kijiji cha Vikuge walionufaika na mpango wa PSSN na kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF.
Mwakilishi wa USAID, Daniel Moore akinunua kitamba cha Batiki kutoka kwa wanufaikaji wa mpango wa PSSN unaoendeshwa na TASAF wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya TASAF mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume wakimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Vikuge aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kufanya biashara ya kilimo cha matunda na mazao mbalimbali. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Vikuge,Vitus Mchami, anayefatia Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare
Baadhi ya Biashara za wananchi wa Vikuge walionufaika na mpanngo wa PSSN wa TASAF.
Baadhi ya wanakijiji wa Mwanabwito, Kibaha mkoa wa Pwani waliohudhuria mkutano wa washirika wa maendeleo.
Mratibu TASAF wa wilaya ya Kibaha, Goodson Hare akizungumza jambo wakati wa kutizama biashara zinazofanywa na wajasiriamali walionufaika na mpango wa PSSN wa TASAF kutoka kijiji cha Vikuge, Kibaha.
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) wakiwasili kwenye kijiji cha Mwanabwito.
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini na viongozi wa TASAF katika picha ya pamoja walipotembelea shamba la miti katika kijiji cha Mwanabwito mkoani Pwani.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (katikati) akifafanua jambo kwa baadhi ya wajumbe wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini wakati wa ziara hiyo.